IDADI KUBWA YA WAGONJWA WA MALARIA NI WATOTO

Na Anita Balingilaki ,Itilima

UGONJWA wa malaria bado unatajwa kusumbua zaidi watoto wa chini ya miaka mitano wilayani Itilima mkoani Simiyu.

Hayo yamesemwa leo na mganga mkuu wa wilaya ya Itilima Dkt Anold Musiba wakati akitoa taarifa ya hali ya malaria wilayani hapo kwenye zoezi ugawaji wa vyandarua vilivyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la world vision Tanzania lililofanyika kwenye kata ya Chinamili iliyopo wilayani hapo.

Kaimu meneja wa kanda ya Nzega kutoka world vision Tanzania  ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Kanadi Nyamoko George. 
 

 Aidha ameongeza kuwa wa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 wagonjwa wa  malaria wa nje (OPD) walikuwa 9,764 kati yao   watoto 4159  sawa na 43%  ambao wapo chini ya umri wa miaka mitano,mwaka 2018 wagonjwa walikuwa 6,209 huku watoto wakiwa 2,460 sawa na 40% ambao wapo chini ya umri wa miaka mitano.

Hata hivyo ameongeza kuwa kwa mwaka 2019 wagonjwa wa malaria wa nje (OPD)  walikuwa 6432 ,watoto chini ya miaka mitano wakiwa 2693 sawa na 41% na kwa mwaka 2020  kuanzia januari hadi julai wagonjwa walikuwa 3088 ambapo watoto chini ya umri wa miaka mitano wakiwa 1449 sawa na 46.9% .

Pamoja na hayo ameongeza kuwa kwa mwaka 2017 wagonjwa waliolazwa kutokana na kuugua ugonjwa huo walikuwa 308 ,watoto chini ya umri wa miaka mitano wakiwa 97 sawa na 31.7%  mwaka 2018 waliolazwa walikuwa 245  huku watoto wakiwa 106 sawa na 43.2% mwaka 2019 waliolazwa 367 ambapo watoto walikuwa 127  sawa na 34.6% .

 "waliofariki kwa ugonjwa  wa malaria kwa mwaka 2017 walikuwa 12  mwaka 2018 walikuwa 3 ,mwaka 2019 walikuwa 5 na  kuanzia januari hadi julai kuna jumla ya vifo 6 na kiwango cha maambukizi kwa wilaya ya Itilima kipo kwa 5.1%"  alisema  Dkt Musiba.

Baadhi ya kina Mama wakiwa na watoto wao.
 

Hata hivyo amesema kuwa katika mapambano dhidi ya malaria  halmashauri imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kutoa elimu / kuhamasisha wananchi kufuata kanuni  na njia mbalimbali za kujikinga na ugonjwa huo kwa kutumia vyandarua vyenye viuatilifu , upuliziaji wa viuadudu vya ki baiolojia kwenye maeneo yenye mazalia ya mbu ,kutoa tiba kinga kwa kinamama wajawazito na kusafisha maeneo ya makazi ili  kuharibu mazalia ya mbu waenezao malaria.

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Itilima Benson Kilangi katibu tawala wa wilaya hiyo  Philibert Kanyilizu amewaomba wadau  waendelee kujitokeze kupambana na kuunga juhudi za kutokomeza ugonjwa wa malaria na hatimaye kuutokomeza kabisa

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kaimu meneja wa kanda ya Nzega kutoka world vision Tanzania  ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Kanadi Nyamoko George amesema kiasi cha shilingi milioni 38,676,000 kilichotolewa na wafadhili kimetumika kununulia vyandarua vyenye viuatilifu vinavyidumu kwa muda mrefu vipatavyo 6,160 ambavyo vimegawiwa kwa watoto wafadhiliwa 3,431 na wasio fadhiliwa 2,729 kupitia mradi wa world vision.

" shirika la world vision Tanzania linaungana na serikali ya awamu ya tano katika juhudi za kupambana na kutokomeza ugonjwa wa malaria na tunaamin kwa vyandarua hivi 6160 maambukizi ya malaria yatapungua kama si kuisha kabisa tukizingatia mpango mkakati wa wizara kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka 7% hadi chini ya 1% ifikapo 2020 na kuitokomeza kabisa ( zero malaria )  ifikapo 2030.



Wakiongea mara baada ya kukabidhiwa vyandarua vilivyotolewa na world vision Tanzania wazazi na watoto wamesema vitakuwa msaada mkubwa wa kukabiliana na ugonjwa wa malaria

" chandarua kitanisaidia kujikinga na maralia nitasoma vizuri zamani nilikuwa naugua sana malaria maan nyumbani hatukuwa na chandarua mbu walikuwa wakining' ata  ila sahivi maralia basi " alisema Nkumba Masunga mwanafunzi shule ya msingi Nanga B iliyopo wilayani hapo.

Awali tulikuwa tunawapeleka watoto hospitali ukifika unaambiwa ni malaria unapewa dawa anatumia mkurudi nyumbani anang'atwa na mbu tena mnarudi hospitali ugonjwa ni ule ule ...tunawashukuru sana world vision Tanzania kwa msaada huu utatusaidia kujiinua kiuchumi tutafanya kazi na kujiongezea kipata badala ya kutumia muda mwingi na gharama kujitubu maralia " alisema Ngolo Masengo ambaye ni mzazi

MWISHO

Post a Comment

0 Comments