Na Shushu Joel,Maswa
MKUU wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu,Aswege Kaminyonge amewataka wananchi waishiyo katika kijiji cha Buyubi wilayani humo kutunza miundombinu ya maji na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapowabaini wananchi wachache wanaohujumu miundombinu hiyo.
![]() |
Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu,Aswege Kaminyonge akisisitiza jambo kwa wananchi juu ya utunzaji wa miundombinu.(PICHA NA SHUSHU JOEL) |
Hayo yameelezwa na Mkuu huyo wa wilaya wakati akiongea na wananchi wakijiji hicho mara baada ya kutembelea eneo ambalo linapita bomba kubwa la maji linalotoa maji kutoka katika Bwawa la New Sola ambacho ndicho chanzo kikuu cha maji katika mji wa Maswa mara baada ya kupasuliwa nwatu ambao hadi sasa hawajajulikana na kusababisha kuwepo kwa tatizo kubwa la upatikanaji wa maji safi na salama katika kijiji hicho.
Alisema kuwa alipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kuwa wamekuwa na muda mrefu hawapati maji ya bomba yanayosukumwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira MjiniN Maswa(Mauwasa)na alipokutana na uongozi wa Mamlaka hiyo ndipo alipoelezwa kuwa bomba kubwa linalopeleka maji katika kijiji hicho limepasuliwa na watu wasiojulikana.
Alisema kupasua bomba ni kuhujumu uchumi na kuwaonya watu wote wanaofanya vitendo hivyo wakikamatwa watafikishwa katika vyombo vya sheria na hivyo kuuagiza Uongozi wa kijiji hicho na Kijiji jirani cha Dodoma kulilinda bomba hilo kwa nguvu zote.
“Kuharibu miundo mbinu ya maji huu ni uhujumu uchumi na yeyote atakayekamatwa atafikishwa katika vyombo vya sheria kwani kupasua bomba hili ni sawa na kuhatarisha maisha ya watu kwani unawazuia wasipate maji safi na salama hivyo niuagize uongozi wa kijiji cha Buyubi na kijiji jirani cha DAGALIN kulilinda bomba hilo na toeni taarifa kwa jeshi la polisi mtakapobaini mtu au watu wanaofanya
vitendo vya kupasua bomba hili,”alisema. Pia aliwataka wananchi wa kijiji hicho kutumia maji yanayosukumwa na Mauwasa kwa kuvuta mabomba katika nyumba zao kwa ili waweze kupata maji safi na salama kwa matumizi yao ya nyumbani.
Naye Kamanda wa Polisi wilaya ya Maswa,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi(SSP),Leonald Nyaoga amewataka wananchi wa kijiji hicho kutumia vikundi walivyonavyo vya ulinzi shirikishi ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wahalifu na amesisitiza watahakikisha wanawakamata wale wote walioshiriki kuhujumu miundombinu ya maji kijijini hapo.
![]() |
Baadhi ya wananchi wa maswa wakimfuatilia kwa makini mkuu wa wilaya hiyo |
Awali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa,Mhandisi Mathias Nandi alisema kuwa watu wasiojulikana wamekuwa wakihujumu miundo mbinu ya maji kwa kupasua bomba hilo na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi kutopata huduma ya maji safi na salama huku mamlaka hiyo ikitumia gharama kubwa kuliziba bomba hilo.
“Mauwasa tumekuwa tukitumia gharama kubwa sana katika kuziba bomba hili ambalo limekuwa likihujumiwa kwa kupasuliwa hasa nyakati za kiangazi na watu wasiojulikana ila kwa taarifa za awali inaonyesha kuwa wafugaji ndiyo wanaofanya hujuma hii ili kuweza kupata maji ya kunyeshea mifugo na hivyo kusababisha wananchi kutopata maji na kusabisha kutumia maji ya kwenye visima na mabwawa ambayo si safi na salama kwa matumizi ya binadamu,”alisema.
MWISHO.
0 Comments