WANACHUO WA UTUMISHI WA UMMA SINGIDA WAKUNWA NA ELIMU YA AFYA YA UZAZI.

Na Shushu Joel Singida


WANACHUO wa Chuo cha Utumishi wa Umma kilichopo Mkoani Singida wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapatia elimu ya Afya ya Uzazi

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utumishi wa Umma Mkoani Singida wakimsikiliza Afisa vijana mkoa huo(NA SHUSHU JOEL)

Afya ya uzazi kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu ni muhimu sana kutolewa kwani wengi wetu tunaotoka shuleni na hasa vijijini elimu hii tumeikosa kutokana na mila zetu kuwa endapo ukimuuliza mzazi juu ya elimu ya uzazi utaonekana kuwa umeanza tabia chafu.

Akizungumza na Wanachuo hao Kaimu Afisa Vijana wa Mkoa wa Singida Ndg Frederick Ndahani alisema kuwa kutokana na wanachuo wengi kuwa ni vijana ofisi yake kwa msaada wa mkuu wa mkoa waliandaa kongamano maalum kwa ajili ya wanachuo hao.

Aliongeza kuwa elimu iliyotolewa na wataalamu wa  Afya imekuwa msaada mkubwa kwa wanachuo na hasa wengi wao ni mabinti kwani uelewa umekuwa ni wa hali ya juu kwao.

Aidha Afisa vijana huyo amewataka wanachuo hao kuwa mabarozi kwa wenzao wa vyuooni na wale walio majumbani ili kuwapatia elimu mlioipata kutoka kwa Mtaalamu wa maswala ya Afya ya Uzazi.


Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Maria Josephata alisema kuwa elimu waliyoipata ni nguzo na mwongozo mkubwa kwao na wenzao walioko majumbani na vyuo vingine.


Aliongeza kuwa kama kuna uwezekana wizara ya Afya na Elimu wakae pamoja ili waone ni jinsi gani wanaweza wakatengeneza mtaala wa kufundishia masomo kwa wanafunzi.


Pia amempongeza Afisa Vijana wa Mkoa wa Singida Ndg Frederick Ndahani kwa ubunifu wake kwani amekuwa ni msaada mkubwa kwa vijana wa mkoa huo katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo yetu.


"Maafisa vijana mkiwa wabunifu mtatusaidia vijana wengi kuweza kujitambua zaidi kutokana na kutupatia elimu mara kwa mara"Alisema.


Kwa upande wake mratibu wa masuala ya Afya na uzazi kutokea wizara ya Afya Geradi Kihwele alisema kuwa tuliombwa kuja kutoa elimu na hivyo kujionea kuwa elimu hii inahitajika kutolewa kwa wanafunzi kwani inavyoonekana wengi wao bado hawajakomaa kwenye balehe.


Alisema kuwa vijana wanachangamoto nyingi ikiwemo kujihusisha na ngono katika umri mdogo na hivyo unaweza kupata mimba zisizo tarajiwa na hata magonjwa ya zinaa.


MWISHO

0717913670

Post a Comment

0 Comments