"CHANGAMOTO YA WANAFUNZI KUKAA CHINI MKURANGA SASA NI HISTORIA" ASEMA DC.

 Na Shushu Joel,Mkuranga.

MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Filberto Sanga amefanikiwa kutatua changamoto ya ukosekanaji wa madawati kwenye shule za msingi na sekondari mara baada ya kukabidhi madawati zaidi ya 1000 kwa walimu wa kada zote mbili za wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akimkabidhi mmoja wa walimu meza na kitu kwa ajili ya shule za sekondari(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati hayo Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa uwepo wa kiwanda cha kutengeneza madawati katika ofisi yangu kwani kumerahisisha sana zoezi hilo.


Aliongeza kuwa kukamilika kwa madawati haya kumepelekea kutatua kabisa changamoto ya madawati kwenye wilaya yetu .

Mwalimu akijaribishia kukaa kwenye meza hiyo huku Mkuu wa wilaya akimshuhudia (NA SHUSHU JOEL)

"Leo nawakabidhi madawati haya walimu wakuu hivyo niwaombe mkawe na uchungu na pesa zilizotumika kutengeneza madawati hayo hivyo ulinzi na utunzaji wa madawati haya ili yadumu kwa muda mrefu "Alisema Mkuu huyo wa wilaya ya Mkuranga Ndg Sanga.


Mbali na ugawaji huo wa madawati Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanafunzi wote walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanafika shuleni kwa wakati ili waweze kuanza masomo haraka iwezekanavyo.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mbezi Rashidi Selungwi amempongeza mkuu wa wilaya kwa ubunifu mkubwa kwa kuanzishwa kwa kiwanda cha kutengeneza madawati ofisini ambacho kimekuwa ni msaada mkubwa katika wilaya yetu.


Aliongeza kuwa awali tulikuwa tukiwanza ni jinsi gani ambavyo tutakabiliana na utengenezaji wa madawati wa haraka lakini mara baada mkuu wa wilaya kuanzisha kiwanda hicho imekuwa ni neema kubwa kwa watoto wetu huko mashuleni.


Aidha kiwanda hicho kimefungua ajira kwa vijana wetu ambao ni mafundi wa ndani ya wilaya yetu pia kumerahisisha hata kupungua kwa Gharama za utengenezaji wa madawati.

Baaddhi ya madawati yakiwa kalakana yakisubilia kupelekwa mashuleni tayari kwa matumizi ya kutumiwa na wanafunzi (NA SHUSHU JOEL)

Naye Mmoja wa walimu waliokabidhiwa madawati na mkuu huyo wa wilaya kutoka shule ya sekondari ya Dundani .......... alisema kuwa kwa jinsi upatikanaji wa madawati umekuwa chini ya ofisi ya mkuu wa wilaya umesaidia kumaliza changamoto ya ukosekanaji wa madawati kutokana na hapo awali ucheleweshaji ulikuwa ni mkubwa sana.


Aidha Mwalimu huyo amemwakikishia Mkuu wa wilaya kuwa hakuna dawati litakalo halibika kwani shule zinasheria ambazo ni kali kwa mwanafunzi huku lengo likiwa ni kutunza mali za shule.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments