Na Shushu Joel,Chalinze
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amewaeleza wananchi wake kuwa mara tu kutakapomalizika kwa soko jipya katika kata ya Bwilingu wananchi Watanufaika kwa asilimia kubwa sana kutokana na upatikanaji wa ajira na kukuza uchumi wa Chalinze
![]() |
Viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete wakiangalia Soko hilo. |
Akizungumza na umati wa wananchi uliojitokeza kumsikiliza Mbunge huyo alisema kuwa soko hili litainua uchumi wa wilaya yetu kwa kufungua milango ya watu mbalimbali kuingia na kutoka kwenye eneo letu kutokana na bidhaa zitakazokuwa zinaingizwa na zingine kutoka kwenda sehemu mbalimbali .
Hivyo kutokana na mwingiliano huo wa watu katika eneo hilo ukusanyaji wa mapato utaongezeka kutokana na mwongezeko huo hivyo itapelekea serikali kukuza uchumi wake kupitia watu.
Aidha Mhe Kikwete aliongeza kuwa mara baada ya soko hilo kuanza kutumika kutapelekea kufunguka kwa ajira kutokana na uwepo wa watu wengi katika eneo la chalinze kujishughulisha na kazi mbalimbali.
![]() |
Mbunge wa Jimbo hilo akiangalia Ramani za soko hilo sambamba na viongozi hao |
"Soko hili wakati linajengwa kulikuwa na wafanyabiasha wasiopungua 180 ambao walikuwa wakifanya biashara zao na tuliwaomba wapishe ili tujenge soko la kisasa hivyo pindi tutakapoanza naomba watu hao wapewe nafasi ya kipekee ili waone thamani yetu kama tulivyoona thamani yao"Alisema Kikwete.
Aidha Mbunge huyo aliongeza kuwa mpaka sasa soko lipo kwenye hatua za mwisho mwisho na hivyo naamini kufikia mwezi wa Tano mwaka huu wananchi watakuwa wamekwisha anza kufanya biashara zao kwenye soko hili.
Naye Bi Fatma Ally (46)ni mmoja wa wafanyabiashara waliopisha mradi huo wa soko la kisasa kujengwa kwenye eneo hilo alisema kuwa awali walidhani kama wanadanganywa tu kumbe yajayo yanafurahisha kwetu sie wafanyabiashara tuliopisha soko kujengwa.
![]() |
"Uwepo wa Soko hili kutafungua milango mingi kwetu sie wafanyabiashara pia serikali kupata pesa kupitia ukusanyaji wa mapato"Alisema Bi'Fatma .
Kwa upande wake Mfanyabishara wa huduma za pesa kwa njia ya mitandao Iddy Gombelo ameipongeza serikali ya awamu ya Tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli kwa msaada mkubwa ulioutoa kwa wanachalinze kwa kuwajengea soko la kisasa kitu ambacho kilikuwa ni ndoto kwao.
Alisema kuwa juhudi zinazofanywa na Mhe. Mbunge wetu Kikwete zimekuwa na tija kubwa kwa halmashauri yetu ya Chalinze kwani sasa ni sawa na kusema kuwa tumesogezewa fursa za upatikanaji wa kipato kwetu.
Aidha Gombelo alisema kuwa mara tu soko hilo litakapoanza kufanya kazi mzunguko utakuwa mkubwa kutokana na wingi wa watu wa kuingia na kutoka katika eneo hilo.
"Vijana wenzangu sasa hakuna sababu ya kulalamikia ajira za serikali kwani tumesogezewa pesa milangoni mwetu"Alisema Gombelo
MWISHO
0 Comments