Na Shushu Joel,Chalinze
MADIWANI wa halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani imepitisha Bajeti ya kiasi cha shilingi Bilioni 38 kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miradi mbalimbali iliyoanzishwa na wananchi na ile iliyojengwa na serikali ili iweze kuanza kutumika kwa jamii.
![]() |
Diwani wa kata ya Miono Juma Mpwimbwi akimsikiliza mmoja wa wachangiaji katika baraza hilo.(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Mipango wa halmashauri hiyo Ndg Shaabani Mlao alisema kuwa fedha hizo zinakwenda kutatua changamoto zote za miradi kwa wananchi hao.
Aliongeza kuwa Wananchi wa halmashauri ya Chalinze wategemee mabadiliko makubwa kwenye sekta ya maendeleo kupitia makusanyo yetu ya ndani.
Aidha alisema kuwa halmashauri ya Chalinze ni moja ya halmashauri zilizotajwa na Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo kuwa zimekuwa kinara wa ukusanyaji wa mapato ghafi.
![]() |
Picha ya madiwani wa halmashauri ya chalinze wakiwa kwenye kikao cha kupitisha bajeti ambapo kwa pamoja walikubaliana kiasi cha shilingi Bilioni 38 zitumike. |
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Miono Juma Mpwimbwi ameipongeza ofisi za mkurugenzi Mtendaji kwa kuzidi kuongeza ubunifu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani hivyo ni vyema sasa tukaongeza juhudi za kutengeneza miradi kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.
Aidha alisema kuwa bajeti iliyopita inakwenda kuwa mkombozi wa maendeleo kwenye kata na vijiji mbalimbali kwa kuwapeleke wananchi huduma za miradi ya Afya,Miundombinu,Elimu na Umeme.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jofrey Kamugisha amewapongeza madiwani wote kwa kupitisha bajeti hiyo kwa kishindo huko akiwataka kwenda kusimamia miradi yote iliyobainishwa ili ikamilike na iwasaidie wananchi wa halmashauri ya Chalinze.
Pia Kamugisha amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanawahudumia wananchi vile ipasavyo ili waweze kunufaika na uwepo wao kwenye halmashauri ya Chalinze.
MWISHO
0 Comments