MKE WA MBUNGE SAGINI AGUSWA MATAJIRI KUWATUMIA WALEMAVU KUJINUFAISHA

Na Shushu Joel

Mke wa Mbunge wa Jimbo la Butiama, Mariam Sagini ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua watu wanaowatumia walemavu kujipatia manufaa binafsi ikiwemo wale wanaotumia bidhaa zinazozalishwa na walemavu.

Mke wa Mbunge wa Jimbo la Butiama Mama Sagini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watu wenye ulemavu

Marimu alitoa wito huo baada ya kutembelea kikundi cha Tuamke Watu Wenye Ulemavu kilichopo Kata ya Butiama na kukuta, wanatengeneza vikapu ambao walilalamikia vikapu hivyo vikifika sokoni vimekuwa vikibadilishwa jina kuonekana sio wao waliotengeneza.


"Nimesikitishwa kuona mtu kama huyu mlemavu asiyeona anatengeneza vikapu na pochi aina mbalimbali ila bidhaa hii uhalali wake haipo kwake, kwa kuwa kuna watu wakidhachukua hizi bidhaa wanaenda kubadili jina wanapachika ya kwao.


"Naombeni tuwe na roho ya huruma, tuacheni michezo kama hii, hawa watu kama wametengeneza bidhaa tununue bila kubadili jina la aliyetengeneza, tuwaunge mkono bila kuwaminya, niombe pia mamlaka zinazohusika ziwasaidie walemavu hawa wapate hakimili yao" alisema Bi Sagini.

Mke wa Mbunge huyo akisisitiza jambo kwa wananchi na walemavu waliojitokeza kwenye mkutano huo

Kwa upande wake Mlemavu wa macho Joyce Nyabusenyi (55) Mkazi Kata ya Butiama ambaye yupo kwenye kitengo cha ufumaji wa vikapu, amemshukuru mke wa mbunge kwa kuwatembelea na kuwapa elimu ambayo itakayowainua kichumi kwani masoko yatakuwa ya uhakika.


"Mimi nina uwezo wa kuzalisha vikapu 15 kwa mwezi kwa elimu ulonipa naweza kuwafundisha wenzagu wajue ufamaji kisha tuzalishe kwa wingi ili soko letu liwe kubwa, bora na endelevu. Japo kwa sasa ujira wangu ni mdogo kutokana na muda mwingine naumwa ambapo shughuli za uzalishaji zinasimama," alisema.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments