UONGOZI NI KUACHA ALAMA KWA JAMII :SHARIFU.

Na Shushu Joel,chalinze. 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Abdul  Sharifu Zahoro amewataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanaweka alama pindi wanapopewa nafasi za kuwaongozo wanachama wenzao. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bagamoyo Abdul Sharifu akifafanua jambo mbele ya viongozi wa chama na serikali juu ya kuipandisha zahanati ya Ubena kuwa kituo cha huku pia akisistiza kuongezwa kwa watumishi(NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wanachama na viongozi wa chama hicho katika kwenye kilelecha kuzaliwa kwa ccm ambapo kiwilaya maadhimisho hayo yalifanyikia katika  kata ya Ubena Halmashauri ya Chalinze.


Aliongeza kuwa wananchi walio wangi wanahitaji kuona kero zao zinatatuliwa na sio kuwafanyia porojo ndio wakuchague hivyo kila kiongozi aliyepewa dhamana na wananchi anapaswa kujitathimini kama yupo tayari kuwatumikia wananchi wanyonge kwa kupambana na shida zao.


"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekuwa ni kiongozi wa mfano mkubwa Afrika na Dunia kwa jinsi ambavyo amekuwa akijitolea kwa wananchi wake hivyo Rais huyu ataacha alama kubwa hapa nchini "Alisema Sharif.


Aidha alisema kuwa wakati anaingia kwenye uongozi wa chama aliwaahidi mambo mengi sana wana ccm wa wilaya ya Bagamoyo ikiwemo ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi katika halmashauri ya chalinze leo nafuraha kusema ujenzi huo umeanza na utakamilika.


Mbali na ujenzi wa ofisi za chama kwenye kata na wilaya pia nimefanikiwa kuwaunganisha wana CCM na kuwa kitu kimoja jambo ambalo awali lilikuwa limepotea kwa miaka mingi huku kubwa niliwaahidi wezangu kuwa ccm itakuwa ikishinda kwa kishindo na hili kila mmoja wenu ameliona kwenye uchaguzi uliopita.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya chalinze ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kimange Ismail Msumi amempongeza Mwenyekiti huyo wa chama huku akisema kuwa Sharif ni kiongozi wa vitendo na ndio maana amekuwa akifanikiwa kila jambo lake anawawaahidi wananchi wa Bagamoyo.


Hivyo amewataka viongozi wote kuanzia ngazi za chini kuiga yale yanayofanywa na Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Bagamoyo ili kila mmoja wetu aweze kuwa mfano kwenye utendaji wake wa kazi 


Naye Latifa Kizota ambaye ni Mmoja wa wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Bagamoyo  amemsifu Mwenyekiti wa chama hicho kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa katika chama hicho kwa kujitolea kwa hali na mali katika kukitumikia na kuwaongoza vyema wana Bagamoyo. 

Aliongeza kuwa Umoja, Ujasili na Usubutu wa Sharif ndio nguzo pekee iliyotufanya kuweza kufanya vizuri kwenye uchaguzi mkuu uliomaliza na kufanikisha kukipa ushindi mnono chama cha mapinduzi.


Aidha Bi'Latifa aliongeza kuwa kama ikitokea viongozi tukamuiga mwenyekiti wetu wa wilaya basi naamini kila mmoja wetu atafanikiwa kuacha alama ya utendaji wake ndani ya ccm na jamii kunufaika kwa asilimia kubwa kwenye maendeleo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments