Na Shushu Joel, Busega.
WAZEE wa Kata ya Mkula Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Simon Songe kwa utendaji wake wa kazi kwa wananchi wa Jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Busega Simon Songe akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wake katika kata ya mkula{NA SHUSHU JOEL} |
Wazee hao wametoa pongeza hizo walipokuwa wakizungumza na Mbunge huyo katika viwanja vya sokoni kwenye mkutano wa hadhara.
Akizungumza kwa niaba ya baadhi ya wananchi wa kata ya Mkula Mahangi Luhanya alisema kuwa mbunge amekuwa msaada mkubwa sana katika kata hii kwa ufanikishaji wa miradi ya maendeleo.
"Kata yetu ya Mkula ilikuwa nyuma sana kwenye maendeleo kwa kukosa huduma mbalimbali za jamii kwa kipindi cha miaka mingi"Alisema Luhanya.
Aidha aliongeza kuwa kata ya mkula ilikuwa na changamoto nyingi katika Afya lakini sasa tangu kuchaguliwa kwa Songe tumepokea milioni 50 kwa ajili ya kumalizia zahanati yetu ilishindikana kujengwa kwa uongozi mwingi uliopita lakini huyu kijana kweli katuonyesha njia ya maendeleo .
Kwa upande wake Mzee Bavo (85)alisema kuwa viongozi kama hawa wanaofanya kazi za ujenzi wa maendeleo kwa jamii wanapaswa kulindwa ili wawasaidie wananchi.
Pia alisema kuwa Mhe Songe amefanikiwa kulipatia heshima Jimbo letu la Busega kwa kuhakikisha maendeleo yanakuwepo kila mahali.
"Sie kama Wazee tumeridhishwa na mwenendo wa utendaji kazi wa Mbunge hivyo tunahitaji vijana kama hawa waungwe mkono ili wafanikishe Malengo ya wananchi waliyokuwa wakiyahitaji"Alisema Bavo.
Kwa upande wake Mhe. Mbunge wa Jimbo la Busega Simon Songe amewapongeza wananchi wa kata ya Mkula kwa juhudi zao za kuchangishana mchango kwa ajili ya maendeleo ya kata yetu.
Aidha amewataka kuendelea kumuunga mkono ili kufanikisha maendeleo ya wananchi ambayo wanayahitaji kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za jamii kila pande ya Jimbo letu.
MWISHO
0 Comments