UVCCM MKURANGA WAMTUNUKU CHETI MWENYEKITI WA CCM.

Na Shushu Joel, Mkuranga.

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wamemtunuku cheti cha heshima Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo  Ndg Ally Msikamo kutokana na jinsi ambavyo Mwenyekiti huyo amekuwa mstali wa mbele katika kukipigania chama hicho.

Akizungumza na wajumbe wa mkutano huo mgeni rasmi wa kikao hicho ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana Taifa Ramadhani Mlao alisema kuwa ni sahihi kabisa kwa Umoja huo kumkabidhi cheti cha pongezi Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mkuranga. 


Aidha Milao amemtaka Mwenyekiti wa UVCCM wilaya  ya mkuranga kuhakikisha anawapambania vijana wenzake wanapata mikopo ili waweze kuenda shughuli zao za kila siku.

aye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mkuranga Ally Msikamo amewashukuru vijana kwa kuona mchango wake na hivyo amewataka vijana kujitambua kwani Taifa linawategemea kwa kusaidia kuongoza nchi hii.


Aidha aliongeza kuwa ni vyema sasa mkajikita katika kutafuta vyanzo vyenu vya pesa kwa kuanzisha miradi mbalimbali itakayokuwa na tija kubwa sana kwenu.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wilaya hiyo Ndg Abdallah  Ngwenda alisema sababu iliyopelekea kuwamtunuku Mwenyekiti wa chama cheti cha  pongezi ni kutokana na juhudi zake kubwa ambazo amekuwa akizifanya katika kuhakikisha chama kinazidi kuwa imara.

"Huyu ndiye Mwenyekiti wa pekee na ndiye anayestahili kuigwa kutokana na juhudi zake zote ambazo amekuwa akizifanya katika kukuza chama"Alisema Ngwenda 

Aidha alisema kuwa uongozi ni kuacha alama hivyo Mwenyekiti wetu wa chama Ndugu Ally Msikamo amefanikiwa kuacha alama na bado anaendelea kufanya mambo makubwa katika wilaya ya Mkuranga. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments