UVCCM BAGAMOYO YAMPA TANO RC KUNENGE.

 Na Shushu Joel, Bagamoyo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akimkabidhi cheti cha pongeza Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Bagamoyo Mkwayu Makota(NA SHUSHU JOEL)

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani umempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Comred Abubakar Kunenge kwa utendaji wake wa kazi za kuwahudumia wananchi mbalimbali wa Mkoa huo. 

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Makoto Mkwayu alisema kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa katika Mkoa huu  ni mambo mengi amefanya kwa kipindi cha muda mchache tu.

"Sie kama Umoja wa Vijana wilaya ya Bagamoyo tunempongeza sana Rc Kunenge kwa juhudi zake anazozifanya katika Mkoa wetu kwani amekuwa kama Mwalimu kutokana na kuwa anafundisha na anaonya jambo ambalo tulilikosa kwa kipindi kidogo" Alisema Mkwayu.

Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa Mkuu wa Mkoa amekuwa msaada mkubwa kwa jamii katika kushughulikia masuala ya migogoro  ya Ardhi  ambayo ilikuwa ni sugu kwa jamii.


Hivyo Umoja wa Vijana tunazidi kumuomba Mkuu wetu wa Mkoa Comred Kunenge kuendelea na kasi hiyo kwani Mkoa wetu unaelekea Panye dhamira ya maana kubwa kwa jamii yetu ya Mkoa wa Pwani. 


Naye Ester Mabula amemsifu Mwenyekiti huyo wa Uvccm kwa kuweza kutambua mchango mkubwa ambao umekuwa ukifanywa na Mkuu wa Mkoa na hasa za maendeleo kwa wananchi ambao kipindi kirefu walikuwa na kiu nayo.


Mbali na hilo ni kweli Comred Kunenge amekuwa msaada mkubwa kwa Chama na Serikali katika Mkoa wetu kutokana na ushauri wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa pasipo kuangalia umri wala kipato. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments