Na Shushu Joel.Mkuranga.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka wakulima wote walio kwenye Mkoa huo kuhakikisha wanatumia fursa ya mvua zinzoendelea kunyesha sasa kwa kulima mazao yanayostahimili ukame
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akifikilia jambo (NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza
kwenye kikoa kazi Rc Kunenge alisema kuwa kipindi hiki Mungu ametushushia neema
ya mvua hivyo ni vyema tukatumia nafasi hiyo kulima mazao ya haraka kwa ajili
ya chakula cha familia.
“Ni vyema
tukatumia mvua zinazoendelea kunyesha sasa kupanda mazao yatakayoweza kuvunika
haraka ili tupate chakula kwa mahitaji ya familia zetu”Alisema Kunenge
Aidha
alisema kuwa ni vyema wataalamu wetu wa Ugani mkatumia kipindi hiki ambacho
mvua zinaendelea kunyesha kwenye Mkoa wetu kwenda moja kwa moja kwa wakulima
wetu kuwapatia elimu ya kutosha juu ya kulima mazao ya muda mfupi na yenye tija
kwa wananchi.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bi, Khadija Ally amemshukuru Mkuu wa Mkoa
Kunenge kwa maono yake ya mbali kwa wananchi wa wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla.
Aliongeza
kuwa wilaya ya Mkuranga imekwisha weka mikakati ya kutumia mvua hizi
zinazoendelea kunyesha kwa kuwafuata wakulima na kuwapatia elimu juu ya
kuchangamkia fursa za mvua hizo kulima mazao sitahiki na yenye kukomaa haraka.
“Kwa kweli
Mkuu wa Mkoa Mhe: Kunenge amekuwa msaada mkubwa kwetu kwani amekuwa akitushauri
mambo mengi kwa kusudi la ufanikishaji wa mahitaji ya wananchi yaweze
kufurahianserikali yao chini ya awamu ya sita” Alisema Mkuu wa Wilaya ya
Mkuranga.
Naye Mmoja wa wakulima wa wilaya ya Mkuranga Ngd Mwarami Juma mara baada ya kufanya mahojiano na HABARI MPYA BLOG alisema kuwa tunampongeza Mkuu wa Mkoa kwa jinsi ambavyo amekuwa na jicho la tatu kwa wananchi wake wa Mkoa wa Pwani na hasa katika kuwapambania kuweza kufikia malengo ya maisha mazuri kwa kutuymia Raslimali zetu.
Aliongeza
kuwa elimu ambayo amekuwa akiitoa kwa wananchi wa Pwani ni wazi kabisa kiongozi
huyu anatamani kumuona kila mwananchi wa Pwani ananufaika na Mkoa huo.
Aidha
amewashauri wakulima wenzake kutumia nafasi za mvua hizi kupanda mazao stahiki
na yenye kukomaa haraka ili kuweza kupata mavuna mengi kwa muda mfupi na ndio
maana Mkuu wa Mkoa ametushauri tutumie mvua hizo kujinufaisha kwa kilimo.
MWISHO
0 Comments