WANANCHI KIBITI WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWATOA KIFUNGONI: RC KUNENGE

Na Shushu Joel,Kibiti.

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kwa niaba ya wananchi wa kibiti amempongeza Mhe: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha ujenzi wa daraja la Mbushi Mwera jambalo ambalo wananchi wa maeneo hayo walikuwa kama wapo kifungoni kwa kipindi cha muda mrefu sasa.

Waziri Mkuu Kssim Majaliwa akisikiliza maelezo ya ujenzi wa daraja hilo(SHUSHU JOEL)

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa kwenye ziara Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea taraja hilo ili kujionea namna gani Rais Samia amemaliza changamoto hiyo ilikuwepo tangu tupate uhuru.

 

“Tulikuwa na Changamoto kubwa ya Daraja hapa Mhe Rais ameleta fedha na Daraja hili linejengwa. Eneo  hii ilikuwa haliipitki” Alisema Kunenge

Aidha  Kunenge ameeleza kuwa eneo hili la Mbuchi ni eneo la Kimkakati kwa Uchumi wa Mkoa kwani kuna shughuli kubwa za Kilimo na Uvuvi zinzzofanywa na wananchi kwa ajili ya kujiongezea kipata na uchangiaji wa pato la serikali kwa ulipata wa kodi mbalimbali

 

Mhe: Rais amefanya kazi kubwa hana ubaguzi anatuhudumia na kupeleka huduka kule kwenye Changamoto zaidi.

Waziri Mkuu wakionyeshana kitu na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge(NA SHUSHU JOEL)

“Wilaya za Kibiti na Rufiji shughuli kubwa zinzofanya ni  Kilimo cha  korosho, Mpunga Ufuta. "Tuna Uwekezaji Mkubwa kilimo cha Mpunga Wilaya ya Kibiti" Alisema Rc Kunenge 

Hata hivyo kumekuwa na wimbi kubwa la Wawekezaji kukimbilia eneo hili kwa sababu lina Maji na Ardhi nzuri yenye rutuba

 

Pia Kunenge ameeleza kuwa  Kutokana na Changamoto ya Mabadiliko ya Tabia Nchi Wafugaji Wengi wamehamia Wilaya ya Rufiji na Kibiti, hali inayopelekea Mifugo kuwa mingi kuliko ukubwa wa Ardhi iliyotengwa kwa malisho.

 

Mhe Kunenge ameeleza Mkoa Unaendelea na kutoa elimu kwa Wakulima kufuga Mifugo kulingana na Ardhi ya Malisho. Ameeleza Mkoa unatekelezwa Mpango wa Ranchi Ndogo na wameanza kwa Wilaya ya  kisarawe tuna Ufugaji na kibiti tuna Ufugaji wa Ranchi Ndogo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  ameridhishwa na Ujenzi wa Dajara Hilo amepongeza Taasisi za TANROADS na TARURA kwa kazi nzuri ya Usimamizi na Ujenzi wa Daraja hilo.

 

Ameeleza kuwa Ujenzi wa Daraja hilo ni dhamira ya Serikali ya Kuhakisha inawafikia Wanchi mpaka Vijijini Hivyo ndiyo maana Serikali imeanzisha Wakala wa Serikali wa Barabara Vijijini TARURA ili kumaliza changamoto za barabara kwa wananchi .

Aidha Waziri Mkuu amemwagiza Waziri TAMISEMI  Kushughulikia Ujenzi wa Barabara Unganishi kutokea Mhoro kufika Mbuchi.

Pia amewataka Wananchi kuchangamkia Fursa za Kiuchumi zilizopo katika eneo hilo ili kuweza kujipatia kipato kitachonufaisha familia zao

 

Katika Hatua Nyingine Mhe Majaliwa amewataka Wafugaji kufuga kulingana na Maeneo wanayoyamiliki. Ameelekeza Serikali za Vijiji zitambue Mifugo yote iliyopo na Maeneo yao na Viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya kusimamia kila Mfugaji awe na eneo la kufugia.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa  amekemea Tabia ya mapigano ya Wakulima na Wafugaji na kutaka wachukuliwe hatua kwa mfugaji ambaye hathamini maisha ya wengine.Aidha Mhe Majaliwa ameitaka Halmashauri hiyo kujenga Zahanati kila kijiji kupitia fedha za ndani.

 

Amesisitiza Utunzaji wa Misitu ya Mikoko na kutaka Wananchi wa Mbuchi kutafuta chanzo kingine cha mapato na Biashara kwa Ukataji wa Miti huo utathiri  Mazingira na vyanzo vya Maji.

MWISHO

 


Post a Comment

0 Comments