KATIBU UWT KIBAHA AWAKUMBUSHA WAZAZI MALEZI MEMA KWA WATOTO.

 Na Shushu Joel 

Nurath Mkandawile katibu wa UWT wilaya ya Kibaha Vijijini


KATIBU wa Jumuiya ya Umoja Wanawake Tanzania wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoani Pwani Bi, Nurath Mkandawile  amewasii wazazi kote nchini kutimiza wajibu wao kwa kutoa malezi mema na yenye kuwajenga watoto ili Taifa liendelee kuwa na kizazi imara.


Rai hiyo ameitoa ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali.


"Nipende kuwakumbusha wazazi na walezi kuweza kukumbuka misingi ambayo sie tumelelewa hivyo ni vyema na watoto wetu wakawa kwenye misingi iliyo na weredi kwa Taifa letu" Alisema Mkandawile 


Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na nia njema na watanzania wote kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo inakwenda kuwa mkombozi wa Taifa letu.


Naye Mwajuma Ally ni mmoja wa wajumbe wa jumuiya hiyo amempongeza   kwa maona yake makubwa kwa uongozi wa jumiuya hiyo kwani katibu amekuwa msaada mkubwa kwa jumuiya yetu.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments