Na Julieth Ngarabali
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imeelekeza wamiliki wa shule mbalimbali zinazotoa huduma za usafiri kwa wanafunzi wake kuhakikisha kwa sasa Kila gari linalobeba watoto hao linakuwa na mhudumu wa kike na kiume na pia iwe na vioo angavu na sio vya giza marufu Tinted .
![]() |
Moja ya magari yakionekana kwa mbali |
Maelekezo hayo yametolewa kupitia waraka uliotolewa na Wizara hiyo na kusainiwa na Kamishma wa Elimu Dk. Lyabwene Mutahaba na kwamba ameeleza watumishi hao wawe waaminifu kwenye magari ya wanafunzi
Pia waraka huo, umetaka magari yanayosafirisha wanafunzi kuwa na vioo angavu badala ya Giza (tinted) kama zilivyo sasa kwa magari mengi yanayotumika kwenye shule mbalimbali.
Katika waraka huo imewekwa wazi kwa mmiliki wa shule atakayeshindwa kutekeleza hilo, anapaswa kutoa taarifa ya sababu ya kushindwa kwa wathibiti ubora.
Utekelezaji wa maelekezo hayo, kwa mujibu wa waraka huo unapaswa kuanza kabla ya muhula wa pili wa masomo kwa mwaka 2023.
Ikumbukwe kwamba idadi kubwa ya wanafunzi wanaotumia mabasi ya shule maarufu school bus ni watoto wenye unri wa kuanzia miaka mwili na nusu (2.6/12) na kuendelea ambao baadhi husoma elimu ya awali na wengine elimu ya msingi.
Maelekezo mengine ni kuacha kuweka miziki, picha na video zinazokwenda kinyume na maadili na badala yake, ziwekwe zinazojenga maadili na uzalendo kwa watoto .
Kufuatia waraka huo, wazazi Mkoani Pwani wamepoteza Serikali kwa namna inavyoendelea kutafuta uvumbuzi wa kukomesha kabisa matukio ya ukatili kwa wanafunzi wanapokua kwenye mabasi hayo ya shule.
" Tumekua tukisimia matukio ya watoto wakilawitiwa na ama dereva au kondakta kwenye gari la shule , inawezekana kabisa hali ya kuwa na vioo vya giza tinted ilichangia maana nje hakuna watu waliweza kuona linaloendelea humo, na moja ya hatua nzuri hii Kwa Serikali"amesema Blandika Masawe
Hivi karibuni akitoa hali ya Takwimu za matukio ya ukatili kwa watoto katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2021, Waziri Wizara ya maendeleo ya jamii ,jinsia ,wanawake na makundi maalumu Dkt. Dorothy Gwajima amesema, jumla ya matukio yaliyoripotiwa ndani ya Jeshi la Polisi ni 11,499 ikilinganishwa na matukio 15,870 katika kipindi kama hicho mwaka 2020, sawa na upungufu wa imatukio 4,371 ikiwa na asilimia 27.5.
Mwisho.
0 Comments