Na Shushu Kibaha.
MJUMBE wa kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Mussa Mansour amefanikiwa kukutana na kundi maalum la watu wenye ulemavu katika wilaya ya Kibaha Mkoa Pwani na kuwasaidia mahitaji mbalimbali.
![]() |
| Mjumbe wa halmashauri kuu na kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Mussa Mansour akimpatia sadaka mtoto mwenye ulemavu (NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza
na walemavu hao waliojitokeza kwa wingi katika ofisi zao zilizoko maeneo ya kwa
Mfipa kata ya Kibaha Mansour alisema kuwa kutoa ni moyo na sio utajiri, pia
tumeambiwa na mwenyezi Mungu kuwa tuwakumbuke kwa chochote wenzetu wasiojiweza
na hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa
mwezi wa Ramadhani.
“Ndugu zangu
nawathamini sana ndio maana leo nimekuja kuwapatia futari hii ndogo ili nanyi
mkaweza kula na familia zenu ingawa nilitamani nipite kwenye majumba yenu ili
niwagawie huko naombeni mnisamee sana kwa hilo” Alisema Mansour
Aidha Mjumbe huyo wa kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Pwani amewakumbusha wananchi wenye nafasi hapa duniani kujitoa kwa wale wenye uhitaji ili kuweza kupata baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu wetu pale tunapowasaidia watu wenye mahitaji.
![]() |
| Baadhi ya walemavu waliojitokeza kupokea sadaka kutoka kwa Mussa Mansour |
Aidha Masour
amewalipitia madeni yote waliyokuwa wakidaiwa walemavu hao katika ofisi yao
ikiwemo maji na kuwanunulia matofali elfu moja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi yao na kuwapatia
kiasi cha shilingi milioni mbili zitakazowasaidia katika ofisi yao
Katika zoezi
hilo Masour aliongozana na sheikh wa Mkoa wa Pwani Hamis Mtupa ambapo
amempongeza sana kwa jinsi ambavyo amekuwa akijitoa kwa jamii.
Aidha Sheikh
Mtupa amemtaka Mansour kuendelea na moyo huo wa kujitoa kwa jamii na hasa watu
wasiojiweza kwani anachokifanya sasa ni baraka kubwa kesho .
“Mwenyezi
Mungu anamakusudi makubwa juu yetu kutokana na kwanini mimi ni mzima wa viungo
na wewe ni mlemavu hivyo tuendelee kuwasaidia wenye uhitaji” Alisema Sheikh wa
Mkoa wa Pwani Mtupa
Kwa upande wake katibu wa walemavu Mkoa wa Pwani Mwalimu Bundara amempongeza Masour kwa kuwafuta machozi ambayo yalikuwa yakiwatiririka bila kujua nani ni mkombozi wao.
Aidha
amemtaka aendelee na moyo huo na wao watazidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ambariki na kumjalia kila hitaji la
moyo wake
“Leo
walemavu mbalimbali tumepokea misaada mingi ikiwemo futari ya siku tatu na
fedha hii yote ni neema kubwa kwetu kwani tulikuwa hatujui nani atajitokeza
kutusaidia lakini kumbe Mwenyezi Mungu anamleta Masour Asante sana kwa niaba ya
walemavu” Alisema Mwalimu Bundara.
MWISHO



0 Comments