Na Shushu Joel, Bukombe
WAZEE wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wamemsifu Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Dkt Dotto Mashaka Biteko ambaye ni Waziri wa Nishati na pia ni Naibu Waziri Mkuu kwa jinsi ambavyo amekuwa akijituma kuwatumikia kwa hali na mali kwa kusudi la ufanikishaji wa maendeleo.
![]() |
Dkt Biteko akifafanua jambo katika moja ya picha zake |
Wakizungumza kwenye vikao mbalimbali vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavyo vimekuwa vikifanywa na viongozi wa Chama hicho, Wazee hao walisema kuwa Dkt Biteko amekuwa ni kiongozi wa wa kuigwa katika jamii kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akiishi na wananchi wake.
Bi, Kabula Elikana (72) Mkazi wa kata ya Lunzewe Magharibi mara baada ya kupata nafasi ya kuzungumza na HABARI MPYA MEDIA alisema kuwa Mbunge Dkt Biteko amekuwa ni kiongozi mwenye uchu mkubwa wa maendeleo hivyo Bukombe imekuwa na mabadiliko makubwa kwenye maendeleo mbalimali ambayo hapo awali yalikuwa ni sugu.
" Kwa jinsi Bukombe maendeleo yanavyofanywa na Mbunge wetu Dkt Biteko ni vyema kijana huyu angezaliwa zamani na kuwa kiongozi miaka hiyo basi jimbo letu la Bukombe lingekuwa ni Ulaya ndogo katika maendeleo " Alisema Bi Kabula.
Naye Shija Telemala (78) Mkazi wa kata ya Busonzo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita amemsifu Dkt Biteko kwa utendaji kazi kwa wananchi wa jimbo lake na ndio jambo lemepelekea wananchi kuendelea kumuamini kuwa kiongozi wao wa kuleta maendeleo.
Hivyo amewataka wana Bukombe kuendelea kumpatia muda wa kutosha kwani kwa hali anayoionyesha yajayo katika Wilaya ya Bukombe yanafurahisha sana kwa kizazi kijacho.
Aidha Mzee Telemala amemtaka Mbunge Dkt Biteko kuacha kubweteka katika utendaji wake kwani azidishe upigaji wa kazi kwa Wananchi na atafika mbali katika Taifa hili.
" Hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kumpatia nafasi ya kuwa Naibu Waziri Mkuu ni kutokana na hekima na utendaji wake wa kazi" Alisema Telemala
Kwa upande wake Mmoja wa viongozi wa Chama hicho ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Wilaya hiyo Ndugu Hassan Abdallah amewapongeza Wazee hao kwa jutambua thamani ya Mbunge na maendeleo anayoyafanya kwa wananchi wa Bukombe.
MWISHO
0 Comments