“JUMUIYA YA WAZAZI CHACHU YA MAENDELEO YA CCM” MWENYEKITI WAZAZI BUKOMBE

Na Shushu Joel,Bukombe

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Hassan Abdalah amesema kuwa Jumuiya hiyo ni chachu ya maendeleo na malezi bora kwa watoto hapa Nchini.

 Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo alipokuwa akizungumza na wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Bulangwa

Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bukombe Ndugu Hassan Abdalah akisema neno kwenye Mkutano huo (NA SHUSHU JOEL)

Alisema kuwa Jumuiya hii ni  nguzo kubwa katika mambo mengi hivyo kila kiongozi aliye ndani ya jumuiya yetu ni muhimu kuweza kujitafakali kwa kina juu ya uwezo wake wa kuongoza na kusaidia jamii yetu katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo

Aidha amewataka viongozi wa jumuiya hiyo kuendelea kuyasema yale mazuri yanayofanywa na Rais wetu wa jamhuri ya Muungno wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwani maendeleo anayoyafanya yamezidi kuwa msaada mkubwa kwa wananchi waTanzania.

 

“ Sasa hivi kuna mashule, zahanati, vituo vya Afya , miundombinu bora ,umeme, maji na mengine mengi ambayo Rais wetu amekuwa akiyafanya” Alisema Hassan ’

Naye katibu wa ccm wa kata hiyo Edmond Bagelezi  alisema kuwa Mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Bukombe ametuachia deni kubwa wana ccm hivyo tuna mwakikishia tutafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha ccm inazidi kuwa juu kama ilivyo sasa.

Aidha amewataka viongozi kuyafanyia kazi maneno yaliyosemwa na mwenyekiti wa Wazazi ili kuweza kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Pia katibu huyo amempongeza mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa katika ufanisi wa ufanikishaji wa maendeleo katika kata hiyo kwani awali kata hiyo ilikuwa nyuma sana lakini sasa hivi tunaweza kusema kuwa Mhe Biteko  ni mfano wa kuigwa.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments