KATIBU WA CCM BUKOMBE AWAFUNDA VIONGOZI KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MTAA

Na Shushu Joel, Bukombe 


KUELEKEA Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongozi na Vijiji Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Ndugu Leonard Mwakalukwa amewafunda viongozi mbalimbali wa Chama hicho kuanzia ngazi ya Matawi, Shina na kata.

Katibu wa ccm Wilaya ya Bukombe Leonard Mwakalukwa akisomo katiba ya chama kwa viongozi wa matawi na kata (NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza katika kikao kazi hicho Katibu huyo alisema kuwa ni vyema kila kiongozi kuweza kujipanga kuhakikisha anakisemea Chama kwa wananchi ili kila mmoja aweze jua kile kinachoendelea kufanywa na Mbunge wetu wa Jimbo na Waziri wa Nishati pia ni Naibu Waziri Mkuu kwa uletaji wa maendeleo.


"Semina hii ikawe kama mwongozo kwenu kwa ajili ya kuelekea katika uchaguzi ujao na iwe ni ishara ya ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) " Alisema Mwakalukwa katibu wa CCM Bukombe.


Aidha amewataka viongozi hao kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwani wao ndio waajili namba moja.


Kwa upande wake katibu kata wa Uyovu Zaitun Ally amempongeza katibu wa CCM wilaya hiyo kwa kutoa semina kwa viongozi ambao wengi wao walikuwa hawajui majukumu yao.


" Semina hii inakwenda kuwa mwongozo mkubwa kwa watendaji wa matawi na kata wa Chama Cha Mapinduzi kwani tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mtaa na vijiji" Alisema Zaitun. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments