Na Shushu Joel, Bukombe
WANANCHI wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamefurahisgwa na utendaji kazi wa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati pia ni Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Mashaka Biteko.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu akifafanua jambo (NA SHUSHU JOEL) |
Wakizungumza na waandishi wa habari wa HABARI MPYA MEDIA wananchi hao walisema kuwa Jimbo la Bukombe limefanikiwa kuwa na wabunge zaidi ya wanane lakini Mhe. Biteko amekuwa ni Mbunge wa pejee katika kutuletea maendeleo ambayo ndio ilikuwa kiu yetu kuyaona.
Ngw'ashi Masalu (43) ni Mkazi wa kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe alisema kuwa Jimbo hili limeweza kupata maendeleo ya haraka kwenye kipindi cha uongozi wa Mbunge mchapakazi Dkt Biteko kutokana na kiongozi huyo kuwa na moyo wa kuthamini wananchi ambao ni waajili wake.
Aliongeza kuwa Dkt Biteko amefanikiwa kuleta maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya,Elimu,Maji,Miundombinu na Umeme hivyo upatikanaji wa huduma hizi muhimu kwa jamii kumepelekea kila Mwananchi kuendelea kuwa na Imani kubwa nae.
"Viongozi wa mfano wa Dkt Biteko ni wachache sana katika Taifa hili hivyo ni vyema wananchi wa Jimbo la Bukombe tukatambua umuhimu wa kiongozi kama huyu" Alisema Bi Ngw'ashi.
Naye Swed Ally (82) Mkazi wa Bukombe amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo kwa kufanya mambo mazuri ya maendeleo kwa jamii na huu ndio uongozi unaotakiwa na wananchi.
Aliongeza kuwa kwa umri nilionao nimewaona wabunge wote wa jimbo hili na kila mmoja alifanya maendeleo kwa wakati wake lakini Dkt Biteko amewashinda mbali sana kutokana na upatikanaji wa kila huduma za jamii tena kwa muda mchache.
MWISHO
0 Comments