DIWANI NG'HWANI AANDIKA HISTORIA.

 Na Shushu Joel, Bukombe 

DIWANI wa kata ya Katente Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Mhe. Tabu Ng'hwani ameandika historia kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe na wananchi wa kata hiyo.

Diwani wa kata ya katente akiwasalimia wajumbe wa mkutano( NA SHUSHU JOEL)

Historia hiyo imewekwa na Diwani huyo kwa kusoma ilani ya utekelezaji wa miradi katika kata hiyo jambo ambalo limewafanya wananchi kupigwa na butwaa kubwa.


Akizungumza katika zoezi hilo Diwani huyo alisema kuwa kwa kipindi cha uongozi wake miradi mingi imetekelezeka kwa kasi kubwa jambo ambalo limerudisha Imani kubwa kwa Chama chetu cha CCM tofauti na miaka ya nyuma.


"Miradi iliyotekelezwa katika kata ya Katente ni mingi katika nyanja ya Afya,Elimu, Maji, Umeme na Miundombinu " Alisema Diwani Ng'hwani. 


Aidha amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko kwa msaada mkubwa ambao anaufanya katika kata hiyo kwenye sekta ya maendeleo.


Naye MNEC wa Geita Evarist Gervas ambaye ndiye alikiwa mgeni rasmi katika usomaji huo wa utekelezaji wa Ilana alisema kuwa ni vyema kila diwani akasema maendeleo makubwa ambayo yanafanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi .


Aidha amemsifu mbunge wa jimbo la Bukombe Dkt Biteko kwa jinsi ambavyo ameibadilisha Bukombe kwa maendeleo.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments