Na Shushu Joel, Bukombe
MWENYEKITI wa wazazi Taifa Ndugu Fadhili Maganya amewataka wananchi wa wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kuwapuuza wale wote wanaobeza msendeleo yanayofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na Wananchi wa kata ya Uyovu katika uzinduzi wa nradi wa maji uliogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milion 360 Mwenyekiti huyo alisema kuwa watu wasiopenda maendeleo ni wengi kutokana na utendaji wa hali ya juu unaofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha alisema kuwa uwepo wa maji katika kata ya Uyovu unakwenda kumaliza changamoto ya maji kwa wananchi na hasa kina Mama ambao wamekuwa wahaga wa muda mrefu lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa mtatuzi mkubwa wa wa upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali kwenye Taifa letu.
Hivyo amewataka wananchi kuendelea kutunza miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu kwa wananchi wa Uyovu.
Naye Meneja wa RUWASA wilaya ya Bukombe Eng James Benny alisema kuwa wananchi wanaopata huduma ya maji yenye uhakika.
MWISHO
0 Comments