HAJAT MARIAM ULEGA AWASHUSHIA NASAHA NZITO UWT


Na Shushu Joel, Mkuranga 


MJUMBE wa Baraza la Umoja wa Wanawake Taifa ( UWT) na Mbaraza wa Jumuiya hiyo kutokea Mkoa wa Pwani Hajat Mariam Ulega amewasihi Wanawake wa Jumuiya hiyo kupendana ,kusameana na kushirikiana.

Hajat Mariam Ulega akitoa ufafanuzi  kwa wanawake wa wilaya ya Mkuranga ( Na Shushu Joel) 


Rai hiyo ameitoa alipokuwa kwenye Baraza la UWT wilaya ya Mkuranga ambapo amewasisitiza Wanawake kuongeza upendo baina yao kwa yao na ili litapelekea kuongeza ufanisi mkubwa katika jumuiya yetu.


Aliongeza kuwa ni vyema  pale unapokosewa au kukosewa na mwenzoko ukaomba msamaha kwa lengo la kujenga ili tuendelee na mambo mengine ya maendeleo ya kuimalisha jumuiya.


Aidha amewakumbusha Wanawake wa Wilaya ya Mkuranga kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi za kuwa wenyeviti wa Mtaa na vitongoji katika maeneo yao mara baada ya serikali kutangaza nafasi hizo.


"Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kielelezo kikubwa cha maendeleo kwa Taifa letu hivyo kila mmoja wetu anapaswa kuyatangaza mazuri ya Rais" Alisema Hajat Mariam Ulega

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Pwani Zaynab Vullu amempongeza Mbaraza kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada kwa jumuiya ya Wanawake .

Post a Comment

0 Comments