Jitihada za kufufua na kurithisha michezo ya jadi inaendelea katika maeneo mbalimbali hii yote ni kuonyesha utamaduni bado una nafasi kwa jamii.
Akiongea na uhuru fm Mjumbe wa baraza kuu Jumuia ya wazazi Taifa ALLY MANDAI ameeleza mashindano hayo ya mchezo wa bao kwa timu za Mkoa wa Dar es salaam yana lengo la kutafuta vilabu endelevu.
Amesema katika mashindano hayo yanayofanyika kwa kila kata MANDAI BAO CUP kwenye ngazi ya mtaa wa buyuni kata ya Pembamnazi wamejitokeza washiriki 20 na washindi watawakilisha ngazi inayofata.
Mashindano hayo ni sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu JULIUS NYERERE kuelekea madhimisho ya kifo chake Oktobar 14 mwaka huu.
0 Comments