Na Shushu Joel,Bukombe
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Geita Mhe. Rose Busiga amegawa mashuka ,kanga ,sabuni na mabeseni kwa ajili ya wazazi katika hospital ya wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ili viweze kuwasaidia kina mama na hospital kwa ujumla.
![]() |
Mhe Rose Busiga Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Geita akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Runzewe Mashariki( NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Mhe. Busega alisema kuwa amefanya hivyo ni kutokana na upendo mkubwa alionao kwa wanawake ambao ndio walimuwezesha kwenda Bungeni kuwasema changamoto zao.
Aidha Mhe. Busega amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha huduma za Afya zinakwisha katika jamii.
Aidha amewaomba wananchi wa Bukombe kuhakikisha wanamlinda na kumpa ushirikiano mkubwa mbunge wao ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko kwani maendeleo ni makubwa katika jimbo la Bukombe.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dr. Deograsia Mkapa amemshukuru Mbunge huyo wa viti maalum kwa jinsi ambavyo amejitolea kwenye hospital yetu ya wilaya kwa misaada mbalimbali aliyoitoa kwa hospital na wagonjwa.
Aidha Dr. Mkapa ametoa wito kwa jamii kujitolea kama alivyofanya Mbunge Mhe. Busiga.
MWISHO
0 Comments