Na Shushu Joel, Kibaha.
TREN ya Mwendo kasi ambayo imeanza usafirishaji wa abilia kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma inakwenda kuchochea ukuaji wa uchumi nchini kwa kasi kubwa
Haya yameelezwa na Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Taifa na Mbaraza wa UWT Mkoa wa Pwani Hajat Mariam Ulega alipokuwa akizungumza na Wanawake wa wilaya ya Kibaha katika kongamano la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aliongeza kuwa kuanza kwa safari za Tren hiyo kunakwenda kuongeza kwa upatikanaji wa fedha ambazo zinatokana na uwingi wa watanzania walio wengi kutumia usafiri huo wa haraka .
Aidha amewataka watanzania walio karibu na Reli ya Tren hiyo inapopita kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo nazo zimekuja mara baada ya kuanza kwa safari hiyo ya SGR, Hivyo pia ni vyema kila mmoja kuwa mwangalizi wa mwenzake katika ulinzi wa Miundombinu ambayo imeigharimu serikali fedha nyingi kwa ajili ya watanzania kuweza kutumia mradi huo.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilaya ya Kibaha Mama Mgonja amempongeza Hajat Mariam Ulega kwa jinsi ambavyo amekuwa nguzo muhimu katika jumuiya ya Wanawake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya UWT Mkoa wa Pwani.
MWISHO
0 Comments