BUKOMBE YATEKELEZA AGIZO LA M/KITI WAZAZI TAIFA


Na Shushu Joel, Bukombe 

AGIZO la alilolitoa Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndg Fadhil Maganya wilaya ya Bukombe Mkoani Geita limetekelezwa kwa vitendo ndani ya Wilaya hiyo.


Akizungumza kwa niaba yake Mwenyekiti Taifa Mwenyekiti wa Wazazi Wiaya ya Bukombe Mkoani Geita Hassan Mohamed alisema kuwa agizo alilolitoa Mwenyekiti Taifa tumelitekeleza kwa vitendo kwa kumkabidhi Ndugu Isaya  Francis baiskel ya miguu mitatu.


Alisema kuwa Mwenyekiti wa Wazazi Taifa alipofanya ziara Bukombe alikutana na mlemavu huyo na kuomba baiskel ya miguu mitatu ili iweze kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.


Aidha Mwenyekiti huyo wa Wilaya amemtaka mlemavu huyo Ndugu Isaya kutumia baiskel hiyo kwani itamsaidia kwenye mambo yake ya kila siku.

Hivyo amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko kwa msaada wa Baiskel hiyo jambo ambalo limeipa heshima kubwa jumuiya.


Pia Mwenyekiti Hassan amewakumbusha viongozi wa jumuiya hiyo kushiriki kikamilifu zoezi la uchaguzi wa serikali za mtaa ambalo linafuka moshi.


Kwa upande wake Ndugu Isaya Francis amekipongeza chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.


Aidha amempongeza Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko kwa kuwa mtekelezaji wa vitendo kwani nitaitumia baiskel hii kuniwaisha kwenye shughuli zake za kila siku. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments