Na Shushu Joel, Bukombe
MCHUANO mkali umefanyika baina ya timu ya Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe Dkt Doto Biteko ambaye ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu dhidi ya Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani katika kiwanja cha Kilimahewa wilayani Bukombe
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Msaidizi wa Mbunge wa Bukombe Ndugu
Jonathan Mgaya alisema kuwa mchezo huo ulikuwa ni ahadi ya Mhe Naibu Waziri kuwa mshindi wa KNK CUP atakutana na mshindi wa Karagwe huku lengo likiwa ni kudumisha mahusiano .
" Mchezo umefanyika kwa ufanisi sana huku pande zote zikionyesha ufundi wa hali ya juu kwa kusakata kandanda Hivyo mpaka mpaka mpira unamalizika hakuna mbabe" Alisema Jona.
Kwa upande wake Mgeni rasmi wa mchezo huo Ndugu Ally Mketo ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo amewapongeza viongozi hao kwa kutimiza ahadi zao kwa wanamichezo.
Aidha Mketo amewataka vijana kutumia fursa hiyo ya michezo kuweza kuonyesha vipaji vyao kwani wanaweza kupata nafasi ya kuzichezea timu kubwa za hapa nchini kama Yanga ,Simba na nyingine na hata nje ya Nchi.
MWISHO
0 Comments