TAKUKURU BUKOMBE YAWAPIGA MSASA WENYEVITI WAPYA


Na Shushu Joel, Bukombe 


TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imewapiga msasa wenyeviti wa Vijiji,Vitongoji na wajumbe wao katika kata ya Lyambamigongo kwa kusudi la kutambua  viashilia vya Rushwa katika shughuli zao.


Akitoa elimu elimu hiyo Afisa wa Takukuru Ndugu Barnaba  Mushi alisema kuwa ni vyema kila mmoja wetu kutambua rushwa ni adui wa haki na Mwenye kurudisha maendeleo nyuma.


Aidha Mushi amewatahadharisha viongozi hao juu ya Rushwa na kuwataka kuachana nayo kwani hata vitabu vitakatifu vinazuia Rushwa.


"Kazi ya Takukuru sio kukamata kamata watu bali ni kuelimisha juu ya maadili mema ya utumishi kwa wananchi" Alisema Mushi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Lyambamigongo Ndugu Obeid Philimon  ameishukuru TAKUKURU  kwa utoaji wake wa elimu kwetu kwani imetufungua na kutufanya tuwe wenye maono mengi katika kuwatendea kazi wananchi waliotupatia dhamana ya kuwaongoza.


Pia ameitaka taasisi hiyo ya kupambana na Rushwa kuendelea kutoa mafunzo hayo mara kwa mara ili kuweza kujenga kizazi chenye kuichukia rushwa kwa vitendo.


Aidha aliongeza kuwa wengi wetu tulikuwa tunajua kuwa Rushwa ni upokeaji wa fedha tu kumbe zipo Rushwa za aina nyingi hivyo uelewa huo unaenda kwenda kuwa chachu ya maendeleo katika sehemu zetu za utawala.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments