MBUNGE BAGAMOYO ASISITIZA UTUNZAJI MAZINGIRA


Na Shushu Joel, Bagamoyo 


MBUNGE  wa Jimbo la Bagamoyo Mkoani Pwani Mhe Muharami Mkenge amewataka wananchi wa Jimbo hilo kuwa mstali wa mbele katika utunzaji wa mazingira ya maeneo ya kwa kufanya usafi.

Mhe Mkenge akishiriki zoezi la usafishaji wa mitaro katika mitaa ya mji wa Bagamoyo ( Na Shushu Joel) 


Rai hiyo ameitoa alipokuwa akishiriki zoezi la usafi wa mazingira katika mitaa mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo kwa kusudi la kuoweka Bagamoyo kwenye muonekano wenye kuvutia.


Mhe Mkenge alisema kuwa ni vyema kila  mwananchi akashiriki kwa moyo ili Bagamoyo ya zamani iweze kurudi na kuendelea kuwa kuvutio na kuongeza thamani ya mji wetu katika sekta ya utalii.


Aidha Mhe Mkenge amewapongeza wote waliojitokeza katika zoezi la usafi wa mazingira wakiwemo wanafunzi ,Bodaboda na wengine wote.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Selenda Shauri amempongeza Mbunge Mhe Mkenge kwa kuwa mstali wa mbele kwa kupambana na mazingira katika Bagamoyo yetu.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments