TAKUKURU RAFIKI NI MKOMBOZI WA WANANCHI" MKUU WA TAKUKURU PWANI


Na Shushu Joel, Kibaha.


TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imefanikisha kusikiliza kero mbalimbali katikq kata kumi na moja (11) za Mkoa huo na kuzitatua kwa kufanikisha hitaji Lao.


Akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Ndugu Alli Sadiki alisema kuwa tangu kutambulishwa kwa TAKUKURU RAFIKI miradi mingi imefanikuwa kumalizika na kuanza kutumika kwa jamii hii ni kutokana na utoaji wa elimu na kuwafikishia wahusika na kuyafanyia kazi

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Ndugu Alli Sadiki akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (Na Shushu Joel) 


Aidha Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa huo alisema kuwa miradi 52 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 12..9 katika sekta ya Afya,Elimu,Maji na Barabara hakukuwa na mapungufu ya aina yeyote ile huku miradi mingine ikiendelea utekelezaji wake.


Aliongeza kuwa pia Takukuru Mkoa wa Pwani imefanikiwa kutoa elimu kwa Umma kwa kutoa semina 60, mikutano ya hadhara 65,vipindi vya Redio 5, uandishi wa makala 12 yote hii ni kwa lengo la kuufikia Umma.


Pia Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa wa Pwani Ndugu Sadiki amesema kuwa  Takukuru itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kuweza kusaidia  miradi ya serikali iweze kuendelea kusaidia wananchi.


Kwa upande wake Mwandishi wa habari wa HABARI MPYA MEDIA ameipongeza Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuanzisha kwa Takukuru Rafiki kitu ambacho kimekuwa suluhisho kwa jamii.


Aidha ameitaka Takukuru kuendelea na utoaji elimu kwa jamii kwani  matokea chanya yamefanyi.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments