Na Shushu Joel, Pwani
MJUMBE wa Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa na Mbaraza wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Hajat Mariam Ulega amesikitishwa na kifo cha kiongozi wa kanisa katoliki Dunia Papa Francisko .
Akizungumza kwa njia ya simu na Mhariri wa HABARI MPYA MEDIA alisema kuwa kiongozi huyo wa kanisa Katoliki alikuwa ni Mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani Duniani kote.
Aidha amewataka wakatoliki wote Duniani kuendelea kuwa na moyo kwani kipindi hiki ni kigumu sana kwao hii ni kutokana na kiongozi huyo alivyokuwa na moyo wa pekee.
" Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi" Alisema Hajat Mariam Ulega
MWISHO
0 Comments