BENKI YA NMB YASHUSHA NEEMA MAGU
Na Shushu Joel
Benki ya NMB imetoamsaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya
Sh200milioni katika wilaya ya magu mkoani mwanza.
Misaada iliyotolewa na benki hiyo inayoongoza kwa kutengeneza faida kati ya benki zote zinazofanyabiashara nchini ndani ya miezi mitano mwaka huu,
inahusisha vifaa vya ujenzi, madawati na vifaa vingine vinavyowezesha ukamilishaji wa miradi ya afya,elimu na usalama waraia.
Benki ya NMB imeshatoa msaada wa vifaa vyenye thamaniyazaidiyaSh
200 milionikwamikoaya Kanda ya Kati.
Akifafanua kuhusu misaada hiyo wakati akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida,
Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB,Nsolo Mlozi, alibainisha kuwa misaada hiyo ni ya zaidi ya
Sh200 milioni iliyotolewa imelenga sekta ya elimu,afya na majanga kwa mikoa mitatu ya
Kanda ya kati.
Akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,
MkoaniSingida, katika shule ya Sekondari ya New Kiomboi, Mlozi alisema fedha hizo zilizotolewana
NMB zimetumika kununua madawati,viti vya shule za sekondari,vitanda na vifaa tiba kwenye sekta ya afya.
Aidha,
alisema lengo la misaada hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali.
Pia alisema misaada hiyo imekabidhiwa kwa baadhi ya shule,zahanati,hospitali katika mikoa ya Singida,Dodoma
na Manyara.
![]() |
Mkuu wa wilaya ya magu mkoani mwanza Dk Philimon Sengati aliyevaa miwani akipokea baadhi ya vifaa toka kwa meneja wa NMB kanda ya ziwa(NA SHUSHU JOEL) |
Pia
NMB walikabidhi madawati 250 na vitanda 80 vyenye thamani ya zaidi ya Sh29.5 milioni kwa baadhi ya shule za Wilaya ya Iramba mkoani humo.
Katika hatua nyingine, Benkihiyo imevipatia kituo cha PolisiWilaya ya Kilosa mkoani Morogoro pamoja na shule ya msingi Msowelo mabati
160 yenye thamani ya Sh5milioni kwa ajili ya kuezekea maboma.
NMB
iliamua kutoa msaada huo ikiwa ni mpango wakuzipunguza baadhi ya changamoto kwa taasisi za serikali hapa nchini,
Menejawa NMB kanda ya mashariki, Baraka Ladislaus,alisema na kubainisha kuwa msaada huo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ili kusaidia kuinua miradi
ya maendeleo.
Baraka
alisema kuwa kati ya mabati hayo, kituo cha polisi wilaya kimepata mabati 80 huku shule ya msingi Msowelo nayo ikipata mabati
80.
Mabati hayo yatasaidia kumalizia ujenzi kwa majengo ambayo ujenzi
wake unaendelea.
“NMB
imekuwa ikiunga mkono miradi ya maendeleo iliyoibuliwa na jamii ambapo tumekuwa
tukiwezesha vifaa vya kuezekea katika sekta ya elimu na afya lakini na miradi
mingine ya kijamii katika mpango wa benki hii kurejesha faida kwa jamii,”alisema Baraka.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Polisi wilaya ya Kilosa, Mayenga Mapalala, alisema msaada huo wa NMB
utasaidia kumalizia ujenzi wa majengo ya kuhifadhi silaha na mahabusu.
“Kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro,
WilbroadMutafungwa,tunashukurukwamsaadahuuwamabatiambayoyatasaidiakumaliziaujenziwavyumbaambavyovitatumikakuhifadhiamahabusu
na amali kwa ajili ya utunzaji wa silahakatikakituochetukipya cha polisiwilayahapaMabwelebweli,”alisemaAfandeMapalala.
![]() |
Mkuu wa wilaya ya magu Dk Philimon Sengati akifafanua jambo mara baada ya kupokea msaada huo(NA SHUSHU JOEL) |
Naye Afisa elimu ya msingi wilaya ya Kilosa,
Christina Hauli,alisema kuwa shule ya msingi Msowelo imekabidhiwa mabati 80 ambayo yatasaidia
kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa na kupunguza adha
ya watoto kurundikana darasani.
Christina
alisema kuwa shule ya msingi Msowelo inakabiliana na changamoto mbalimbali
ikiwemo upungufu wa walimu na vyumba vya madarasa kutokana na shule hiyo kuwa
na idadi kubwa ya wanafunzi.
Wakati huo huo,
wakazi zaidi ya 6,000 wa kijiji cha Nsola Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wamepata
matumaini ya kuondokana na adha ya kutembea umbali wa kilimoita 11 kufuata
huduma ya afya kijiji jirani cha Bubinza baada ya Benki ya NMB kuwapatia vifaa
vya ujenzi vyenye thamaniya Sh20 milioni vitakavyotumika kukamilisha ujenzi wa zahanati kijijini hapo.
PamojanavifaahivyovilivyokabidhiwakwaMkuuwaWilayayaMagu,
Philemon Sengati, Meneja wa NMB Kanda yaZiwa, Donatus Richard,alisemabenkihiyo
pia imechangia madawati 130 yenye thamani ya Sh10 milioni kwa ajili ya shule za
msingi za Matela na Muda za wilayani humo na hivyo kufanya misaada yote kuwa na
thamaniya Sh30 milioni.
“Huu
ni utekelezaji wa sera ya kurejesha sehemu ya faida kwa jamii. Kwa mwaka 2020,
NMB imetenga zaidi ya Sh1 bilioni kuchangia miradi ya maendeleo katika sekta za
afya na elimu na hivyo kuwa
benki inayoongoza kwa kuchangia miradi ya maendeleo nchini,” alisema Richard.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu misaada hiyo,
Lucia Abel na Julius Magigima ambao ni wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika kijiji cha
Nsola, walisema ujenzi wa zahanati kijijini hapo tutaondokana naadha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya kijiji jirani, bali pia utapunguza vifo vya mama
wajawazito na watoto wachanga.
“Kwa
sasa, wajawazito kutoka kijiji cha Nsola wanatembea kwa miguu au kutumia
usafiri wa baiskeli kufuata huduma ya kliniki katika Zahanati ya Bubinza,
umbaliwakilomita 11.
Adha hii itaisha zahanati hii ikikamilika. Tunaishukuru NMB
kwa mchango huu,” alisema Lucia.
MWISHO…
0 Comments