Na Anita Balingilika
JUMLA ya kiasi cha shilingi milioni 249.4 zimetumika kwenya uchimbaji wa kisima na ujenzi wa jengo la huduma ya tiba na matunzo (CTC) na ukarabati wa zahanati ya old maswa inayomilikiwa na kanisa katoliki iliyopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Uchimbaji wa kisima umegharimu kiasi cha shilingi milioni 39, 533,540 ambazo zinahusisha uchimbaji wa kisima na ukarabati wa matenki na mabomba ambayo yalikuwa yameharibiwa na kutu ambayo awali miundombinu hii ilitumika kuvuna maji ya mvua huku kiasi cha shilingi milioni 209,885,665 kikitumika kwenye ujenzi wa na ukarabati wa majengo ya zahanati ya old maswa fedha ambazo zimefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Doctors with Africa (Cuamm)linalofanya kazi na mkoa wa Simiyu kama mdau wa afya katika masuala ya UKIMWI na huduma za afya ya mama na mtoto.
![]() |
Makamu Askofu jimbo katoliki Shinyanga padre Kizito Nyanga akiongea kabla ya uzinduzi wa jengo jipya la huduma ya tiba na matunzo (CTC). |
Hayo yamesemwa jana na mganga mfawidhi wa zahanati ya old maswa Dkt Ndaro Lawi wakati akisoma risala ya uzinduzi wa jengo jipya la huduma ya tiba na matunzo (CTC )lililopo kwenye zahanati hiyo ambayo mpaka sasa imendikisha wahitaji wa huduma hiyo wapatao 219.
Padri Paul Kitali ni paroko wa parokia ya old maswa amesema kisima hicho kina uwezo wa kutoa lita 2500 kwa saa huku akiongeza kuwa wananchi wamekuwa wakichangia kiasi kidogo cha shilingi mia tano kwa madumu sita yenye ujazo wa lita ishirini kwa kila moja hatua iliyopelekea kuwapunguzia changamoto ya adha ya maji .
![]() |
Muonekano wa Jengo jipya kwa ajili ya Tiba na matunzo likiwa tayari. |
Akiongea kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa wa mkoa wa Simiyu Festo Dugange, mratibu wa kuthibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi mkoa wa Simiyu Dkt Khamis Kulemba amesema uwepo wa kituo hicho utasaidia sana huku akiwaomba walioanza kutumia dawa za kufubaza virusi vya ukumwi kutoacha dawa kwa kigezo cha kuombewa na kuwa na imani kuwa wamepona kwani kwa kufanya hivyo wanaongeza usugu wa virusi vya ukimwi na kuwafanya kuwa kwenye hatari zaidi .
"baadhi ya madhehebu yanaleta vikwazo katika matibabu ya UKIMWI unakuta baadhi wanasema maombi yanaponya watu wanaacha dawa na kutengeneza usugu wadudu wanakuwa na sugu mgonjwa anazidiwa kikubwa kwa walioanza kutumia dawa endeleeni nazo "alisema Kulemba
![]() |
Kaimu Askofu Kizito akikata utepe kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo. |
Kwa upande wake makamu wa askofu jimbo katoliki Shinyanga padre Kizito Nyanga ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kanisa lina kiu ya kuwafikia watu kwa matendo (huduma ) na lipo tayari kushirikiana na watu wote wanaotoa huduma na ndio maana likafungua mlango kwa cuamm lengo likiwa kuisaidia serikali ya awamu ya tano.
MWISHO
0 Comments