DC SANGA AWATUMBUA WATATU AKIWEMO KATIBU WA CCM.

Na Shushu Joel

MKUU wa wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Philberto Sanga amewatumbua viongozi watatu wa kijiji cha Kibesa kata ya Kisegese wilaya humo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi dhidi ya wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Philberto Sanga akisisita jambo mbele ya wananchi wa kijiji cha Kibesa(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Waliotumbuliwa kwa kusimamishwa kazi ili wapishe uchunguzi wa kamati ndogo aliyoiunda Mkuu huyo wa wilaya ni Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw,Hamis Omary,Mtendaji wa kijiji Bw,Ally Hamis na katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) Bw, Said Kuyawa wote wakituhumiwa kutumia matumizi mabaya ya ofisi,kujichukulia maamuzi yao binafsi bila kushirikisha mikutano ya kijiji,kuuza ardhi ya kijiji na kushindwa kusimamia fedha za miradi ya maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha kibesa wakimfuatilia mkuu wa wilaya ya Mkuranga Philberto Sanga hayupo pichani (PICHA NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza na wananchi hao mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kutokana na tuhuma zinazowakabili watuhumiwa itawabidi wakae pembeni ili wasubili uchunguzi ukamilike.

Aliongeza kuwa anawapongeza wananchi kwa ujasili wao wa kusema ukweli kwa maovu wanayofanyiwa na viongozi hao wasiokuwa na maadili

Mtendaji wa kijiji hicho Bw,Ally Hamis  aliyesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi(SHUSHU JOEL)
"Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli amekuwa akisikitishwa na baadhi ya viongozi wasiokuwa na uadilifu kwa wananchi wanyonge na mimi kama mwakilishi wake sitaki kuona wanyonge wananyanyasika hivyo nitaendelea kuwasimamisha kazi kama mtashindwa kuwasaidia wananchi wanyonge"Alisema Sanga.

Pia Mkuu huyo wa wilaya amemwagiza mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibesa kuilipa mifuko ya saruji zaidi ya 40 iliyotolewa na serikali kwa ajili ya kuweka sakafi kwenye darasa na matokeo yake ikaganda na kupelekea kushindwa kutumika.


Mkuu wa wilaya akipokea malalamiko ya wananchi yaliyowasilishwa na mtendaji wa kata
Aidha katika hatua hiyo mkuu huyo wa wilaya alifanya maamuzi ya kukasimu madaraka kwa kijiji hicho kwa kumchagua Afisa kilimo wa kijiji hicho Said Ngalombo kuwa mtendaji wa kijiji na katika nafasi ya umwenyeki wa kijiji ilichukuliwa na mwanamama Febronia Zabroni huku waliokuwepo wakifanyiwa uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowaandama.

Kwa upande wake Samwel Kimose alimpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kutambua thamani ya wananchi wa kijiji cha Kibesa kwani walikuwa wakiteseka kwa kipindi kirefu kwa viongozi hao kujiona ni Mungu watu.

Aidha amemkabidhi mkuu huyo wa wilaya nyaraka mbalimbali ambazo zilikuwa zikitumiwa na viongozi hao kwa kuuza maeneo mbalimbali ya kijiji huku wakitoa risiti feki.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho ambaye pia ni mwalimu wa shule iliyopo kijiji hapo akichangia hoja kwa mkuu wa wilaya.(SHUSHU JOEL)
Naye Mwenyekiti mpya aliyekaimishwa nafasi hiyo amewapongeza wananchi hao kwa kumwamini na kumchagua kutoka kwenye kamati ya maendeleo ya kijiji ili awe mwenyekiti wa muda.

Aliongeza kuwa umoja,ushirikiano ndio utakao tuvusha kutoka hapa tulipo na kwenda mbele kimaendeleo

Wananchi wakiwa makini kumsikiliza mkuu wa wilaya Sanga(SHUSHU JOEL)
Alisema kuwa kijiji hiki kina wawekezaji wengi lakini wamekuwa wakishindwa kutambulika kwa sababu za upigaji wa viongozi wetu waliokuwepo madarakani hivyo naamini kuondolewa kwao madarakani kutakisaidia kijiji hiki kukua kiuchumi.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments