DC MKURANGA AKABIDHI KUKU WANANCHI.

Na shushu joel

MKUU wa wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Philberto Sanga amewakabidhi wananchi wa wilaya hiyo kuku kwa ajili ya kuanza ufugaji wa kisasa kwa wakazi hao ili kuondokana na umasikini mkubwa uliokuwa ukiwaandana wakazi wa maeneo mbalimbali.


Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Philberto Sanga akimkabidhi mmoja wa washiriki wa mafunzo ya ufugaji wa kuku .
Kuku wamekabidhiwa kwa vijana na vikundi mbalimbali kwa makusudi ya kuwawezesha wakazi hao katika shughuli zao za kukuza uchumi wa wilaya hiyo pia wao binafsi na familia zao.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuwakabidhi kuku 46 kila kijana na kila kikundi Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kuku hawa ni mtaji tosha kwa vijana na vikundi hivyo la msingi ni kuhakikisha wanawatunza ili waje wawanufaisha hapo baadae mara baada ya kuanza kuvuna kuku hao.

Picha ya pamoja ya mkuu wa wilaya,mkufunzi na wanufaika wa mradi wa ufugaji wa kuku.(PICHA NA SHUSHU JOEL






















)
"Kila mmoja wenu anapaswa kutambua hawa kuku anaokabidhiwa ni pesa ya serikali imetumika hivyo serikali ya wilaya itakuwa bega kwa bega kwa kuwafuatilia ili kujua nani ameteketeza pesa ya umma"Alisema Sanga.

Aidha Sanga aliongeza kuwa nchi yetu inauhitaji mkubwa wa nyama nyeupe hivyo wananchi wangu tumieni fursa hii iweze kuwanufaisha katika kukuza uchumi kwa kuzalisha kuku wengi.

Mkuu wa wilaya Sanga akikabidhi kuku kwa wananchi wake huku mkufunzi toka wizara ya mifugo na uvuvi kulia akufurahia(NA SHUSHU JOEL)
Naye Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko kutoka wizara ya mifugo na uvuvi  Felix Nandonde ambaye alikuwa akitoa elimu kwa wananchi wa Mkuranga waliofanikiwa kupata kuku hao aliwataka kuwatumia kuku hao kama daraja la kukuza kipato chao.

"Serikali imejitahidi sana kupambana na ugonjwa wa Mdondo ambao kwa kipindi kirefu ulikuwa unawasumbua sana wafugaji wa kuku kwa kuwaletea chanjo ambayo ni komesha na wote waliokabidhiwa kuku leo wamepatiwa dawa hizo"Alisema Nondonde

Mkuu wa wilaya ya mkuranga Sanga akisissita jambo kwa wananchi walionufaika na mradi wa ufugaji wa kuku
Aidha aliongeza kuwa Wizara imekabidhi kuku zaidi   ya 2000,chakula na dawa za chanjo kwa wilaya ya Mkuranga tu huku wafaidika wakubwa wakiwa ni vikundi na vijana wachache waliojitokeza katika mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mmoja wa wananchi waliopata mafunzo na kupewa kuku Bi, Mery Matolele(51) amewapongeza viongozi wote wa wilaya hiyo na hasa Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kwa jinsi anavyojitolea kwa kuwasaidia wananchi wake wa mkuranga ili kuondokana na umasikini.
Wataalamu kutoka wizara ya mifugo na uvuvi wakiongozwa na Felix Nandonde wakimuonyesha mkuu wa wilaya ya mkuranga Philberto Sanga kuku hao.

Aidha amewahakikishia viongozi na wakufunzi hao kuwa watawatunza kuku hao na watahakikisha wanawatumia kwenye kuwavusha katika uchumi walionao na kwenda wa juu zaidi.

Alisem kuwa wilaya ya Mkuranga wananchi wengi ni wakulima hivyo sie tutakuwa chachu ya kubadilisha zana ya kutegemea kilimo na kuwa wafugaji wa kisasa zaidi.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments