ALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete amefanikiwa kutetea nafasi yake ndani ya chama cha mapinduzi(CCM) kwa Kushinda washindani wake katika kura za Maoni kuelekea uchaguzi Mkuu wa Uraisi, Wabunge na Madiwani uliofanyika katika viwanja vya msata mapema tarehe 20 Mwezi huu.
Mh Ridhiwani Kikwete akizungumza neno mbele ya wana CCM wenzake kabla ya kushinda kura za maoni.(NA SHUSHU JOEL) |
Aliongeza kuwa uchaguzi ulikuwa ni mkali lakini Kikwete ameibuka na mshindi wa kura 369 na kuacha wapinzani wake kwa kura zaidi ya Mia moja.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia uchaguzi wa jimbo la chalinze(NA SHUSHU JOEL) |
Aidha alisema kuwa waliokuwa wakimfuata kwa karibu ni Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno aliyepata kura 273,Said Zikatimu ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze kwa kupata kura 223,Imani Madega 33 na wagombea wengine 21 wakigawana kura zilizobaki.
Mh Ridhiwani Kikwete akipiga kura kabla ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo.(SHUSHU JOEL) |
Naye mmoja wa wapiga kura kutoka kata ya kibindu Amina Juma(46) alisema kuwa uchaguzi umesimamiwa vizuri na wasimamizi walioteuliwa na chama hivyo Kikwete alikuwa ni chaguo la wanachalinze tu.
Mh Ridhiwani Kikwete akisaini mara baada ya kutangazwa mshindi.(SHUSHU JOEL) |
Naye mshindi wa uchaguzi huo Mh Ridhiwani Kikwete ambaye hakutaka kuongea mengi alisema kuwa ushindi uliopatikana ni ishara tosha kuwa wanachama wa CCM wa Jimbo hilo bado wanamuhitajika kuendelea kuwatumikia hivyo amejipanga kutumika kwa maendeleo yao. "....... Kwa ushindi huu wa kura za maoni ni mwanzo tu hivyo tuendelee kumuomba Mungu ili jina liweze kurudi kutoka vikao vya ccm "Alisema.
Baadhi ya wana CCM wakicheza nyimbo za chama hicho kabla ya uchaguzi kufanyika.(SHUSHU JOEL) |
MWISHO
0 Comments