KIKWETE ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU.

Na shushu joel .

ALIYEKUWA  Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh Ridhiwani Kikwete amechukua  na kurejesha fomu kwa ajili ya kuendelea kuwatumikia wanachalinze kwa kipindi kingine cha miaka mitano inayoanza 2020-2025.

Mh mbunge wa jimbo la chalinze anayemaliza muda wake Ridhiwani Kikwete akijaza fomu kisha kurejesha(NA SHIUSHU JOEL)
Mheshimiwa Kikwete ambaye hakutaka kuzungumza mengi mara baada ya kuchukua na kurejesha fomu hizo alisema kuwa wanachama wa CCM wenyewe wanajua yupi ni kiongozi anayewafaa aliyewavusha kwenye changamoto zao zilizokuwa zikiwaandama.
Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo Getrude Sinynza akipokea fomu toka kwa Mh Ridhiwani Kikwete(NA SHUSHU JOEL0
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) wilaya ya Bagamoyo  Bi.Getrude  Sinyinza amewapongeza wote waliochukua fomu kwa majimbo yote mawili yaliyo kwenye wilaya hiyo.


Aidha alisema kuwa kipindi hiki waliojitokeza ni wengi na hii inaonyesha jinsi gani chama hiki kilivyo pendwa na chenye hazina kubwa ya vijana wenye uwezi wa kuongoza na kulisaidia taifa letu.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments