MTUWA AWATOA HOFU WAGOMBEA UBUNGE UVCCM.

Na shushu joel

MSIMAMIZI wa kinyang'anyilo cha kuwania uwakilishi wa nafasi ya ubunge kupitia jumuiya ya vijana(UVCCM) Mkoa wa Pwani Omary Mtuwa amewatoa hofu vijana waliojitokeza kwenye ulingo huo.

Msimamizi wa uchaguzi wa ubunge kupitia umoja wa vijana(UVCCM) mkoa wa Pwani ambaye pia ni katibu wa CCM wilaya ya Rufiji Omary Mtuwa akifafanua jambo (NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo kumalizika Mtuwa alisema kuwa unaweza ukawa mshindi wa kura za hapa mkoani lakini jina lako lisirudi katika vikao vya maamuzi.

"Wagombea wengi wamekuwa na imani kuwa yule anayeongoza kwa kura nyingi ndiye mshindi,hapana chama chetu cha mapinduzi kina utaratibu wa vikao mara baada ya kupeleka majina hivyo vikao ndivyo venye mamlaka juu ya nani anatakiwa kurudi ili kupeperusha bendera ya vijana"Alisema Mtuwa.

Omary Mtuwa msimamizi wa uchaguzi Uvccm mkoa wa Pwani akiwa na Khadija Ismail kulia mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi na Khadija kuongoza kura.(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Aidha Mtuwa aliongeza kuwa vijana wengi wamekuwa na mitizamo ya kutaka kupata tu na si kukosa hivyo nawasihi kuwa wavumilivu kwani ndani ya chama kuna nafasi nyingi na si lazima muwe wabunge bali mnaweza mkapata hata uteuzi kutokana na umri wenu.

"Chama cha mapinduzi (CCM) kinawategemea kwenye kufanya kampeni mara baada ya kutangazwa kuanza kwa uchaguzi mkuu kwa kutumia sifa zenu huko makwenu ili tuweze kupata ushindi wa kishindo kwenye nafasi za Madiwani,Wabunge na Rais"Alisema Mtuwa.

Baadhi ya wagombea wa nafasi ya uwakilishi wa ubunge kupitia jumuiya ya vijana (UVCCM) Mkoa wa Pwani(SHUSHU JOEL)
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uchaguzi huo Christina James ambaye pia ni katibu wa Uvccm mkoa wa Pwani alisema kuwa wagombea waliojitokeza kuchukua fomu ni 18 tu na wote wanasifa za kuwa viongozi hivyo atakyeibuka jina lake kurudi ni lazima tumuunge mkono kama jumuiya.

Akisoma matokea mara baada ya kutoa angalizo la kutokusherekea James alisema kuwa Khadija Ismail amepata kura 15,Mary Joseph kura 8,Mufandii Msaghaa kura 6 na wa nne ni Cstherine Shayo aliyepata  kura 2 huku wengine wakiambulia 1 na wengine 0 .

Khadija Ismail aliyefanikiwa kuongoza kura katika uwakilishi wa ubunge kupitia UVCCM mkoa wa Pwani kabla ya kupata matokeo(NA SHUSHU JOEL)
Aidha Mkurugenzi huyo wa uchaguzi alisema kuwa vijana wanajitambua hivyo ana amini watamuunga mkono yule ambaye jina lake litakayerudi kutoka kwenye vikao vya maamuzi.
Moja wa wajumbe wakipiga kura kwenye uchaguzi huo
Naye Khadija Ismail aliyepata kura 15 na kuwa kinara kwa wagombea alisema kuwa yeye si mshindi bali vikao ndivyo vyenye maamuzi juu ya uwakilishi wangu kwenye nafasi hiyo ya ubunge kupitia vijana.
Msimamizi wa uchaguzi wa UVCCM mkoa wa Pwani kwenye uwakilishi wa nafasi ya ubunge akimkabidhi Mwenyekiti wa jumuiya hiyo karatasi ya kupigia kura.(NA SHUSHU JOEL)
Aliongeza kuwa amependa mfumo wa upigaji wa kura kwani umekuwa wa uwazi hivyo kila mgombea amejionea kile alichopanda.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments