“RAIS MKAPA ATAKUMBUKWA KWA UTETEZI WA KIJINSIA”MKURUGENZI WA TGNP.

Na Shushu Joel
 
MKURUGENZI wa mtandao wa jinsia nchini (TGNP)Bi,Lilian Liundi ameungana na watanzania wote nchini kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamini William Mkapa huku akielekeza kuwa Taifa limepoteza nguzo ambayo ilikuwa mstari wa mbele kwenye masuala ya kuweka usawa wa kijinsia nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi akifafanua jambo.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu za rambirambi mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kipindi cha utawala cha Hayati Mkapa aliweka misingi mikubwa kwa ajili kuendeleza usawa wa kijinsia katika nchi ya Tanzania na kisera,kisheria na kitaasisi pia aliruhusu ushiriki wa makundi mbalimbali katika kufikia misingi ya kijinsia.
“Nakumbuka kipindi wanawake wanarudi kutoka Beijing kitu alichokifanya Mkapa ni kitendo cha kuwapokea wanawake ingawa ndani yao hao wanawake baadhi waliambiwa waishie uwanja wa ndege na ajenda yao ya Beijing lakini Hayati Mkapa aliwapokea wanawake wote waliokuwa wameongozana na Balozi Getrude Mongella”Alisema Liundi
Aliongeza kuwa katika upande wa Azimio la jinsia na maendeleo ukanda wa  SADC Hayati Mkapa alikuwa mstari wa mbele sana katika nchi za SADC, Tanzania zilikuwa moja wapo wa nchi zilizoshiriki kwa kusaini Azimio hilo kwenye kipindi cha uongozi wake  na kufikia kwa asilimia 30.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamini William Mkapa
Aidha aliongeza kuwa katika ngazi ya Afrika,Maputo protocal pia ilikuwa ni kipindi cha Hayati Mkapa ambapo aliridhia mkataba kwa makusudi ya kuendeleza usawa wa kijinsia huku akisema kuwa japo kuna mapungufu lakini kwa kipindi changu lazima utekelezji uwekewe misingi imara zaidi.

Hivyo Liundi alisema kuwa Hayati Mkapa atakumbukwa kwa mambo mengi aliyoyaanzisha hapa nchini na kwa hali hii ni lazima kila mtanzania akimkumbuka machozi lazima yamtoke.
MWISHO

Post a Comment

0 Comments