JESHI LA POLISI LAJIPANGA DHIDI YA WAVUNJIFU AMANI

Na Bahati Sonda, Simiyu.


JESHI la polisi nchini limesema kuwa limejipanga dhidi ya watu waliojipanga kufanya uhalifu katika kipindi hiki cha kampeni na kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika mapema  oktoba 28, mwaka huu huku likihakikisha uchaguzi utakuwa huru na wenye amani.

Hayo yamebainishwa na Naibu Kamishina wa Jeshi la polisi wa Fedha na logistiki, DCP Dhahiri Kidavashari anayesimamia Kanda ya Kagera, Simiyu, Mwanza, Mara na Kanda Maalumu ya Kipolisi(Tarime na Rorya) wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu kwa lengo la kuangalia utayari wa askari kufanya kazi kuelekea kuhusiana na shuguli za uchaguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe akizungumza na waandishi habari kuhusiana na jinsi ambavyo jeshi hilo kwa Mkoa Simiyu walivyojiandaa kufanya kazi kipindi cha kampeni na kuelekea uchaguzi Mkuu(PICHA NA BAHATI SONDA)
 

Aidha Kidavashari aliongeza kuwa jeshi hilo linawataka wananchi kuliunga mkono kwa kutii sheria bila kushurutishwa na kwamba halitosita kuchukua sheria dhidi ya yeyote atakayekiuka na kuvunja sheria huku likiwahakikishia kufanya uchaguzi kwa amani.

"Jeshi la polisi limejiandaa kwa yeyote atakayefanya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kampeni na kuelekea uchaguzi Mkuu, tuko tayari kwa yeyote atakayetuchokoza"

Katika hatua nyingine alisema kuwa tayari jeshi la Uhamiaji limeshahakikisha usalama kwenye maeneo ya mipaka dhidi ya watu wanaoweza kutoka huko na kuja kufanya udanganyifu wa kupiga kura ambapo wao sio raia wa hapa nchini.

 Askari polisi wakionesha umahiri wa mazoezi ya utayari kuelekea kipindi cha uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba 28, mwaka huu mbele ya Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi  wa Fedha na logistiki, DCP Dhahiri Kidavashari.(Picha na Bahati Sonda)
 

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe alibainisha kuwa mpaka sasa mkoa ni shwari na kwamba hakuna taarifa za uvunjifu wa amani huku akitoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwenye jeshi hilo pindi wanapopata au kusikia viashiria vya uvunjifu wa amani.

Mbali na hayo Kamanda Mwaibambe aliongeza kuwa mikutano yote ya vyama vya siasa itasimamiwa na jeshi la polisi huku asisitiza suala la kutoa taarifa kwa mtu atakayeona ametendewa ndivyo hivyo badala ya kufanya fujo.

 Askari polisi wakionesha umahiri wa mazoezi ya utayari kuelekea kipindi cha uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba 28, mwaka huu mbele ya Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi  wa Fedha na logistiki, DCP Dhahiri Kidavashari.(Picha na Bahati Sonda)
 

"Nipende kusema kwamba mpaka sasa Mkoa wa Simiyu hauna taarifa ya uvunjifu wa amani ambapo pia Mikutano yote ya vyama vya siasa inasimamiwa na jeshi la polisi, haijalishi mgombea ana watu wangapi mkutano wake utasisimiwa "Alisisitiza Mwaibambe
 
Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) uzinduzi wa mikutano ya kisiasa ni leo agosti 26, 2020 ambapo itaendelea kufanyika kwa muda miezi 2.

         Mwisho.

Post a Comment

0 Comments