Na shushu joel, Simiyu
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuwa mabarozi wa kutangaza habari na kutoa elimu kwa jamii juu ya magonjwa ya milipuko.
Rai hiyo imetolewa na Mtaalamu wa Magonjwa ya mlipiko Mkoa wa Simiyu Dr Khamis Kulemba alipokuwa akitoa elimu juu ya madhara yanayotokana na magonjwa hayo.
![]() |
Dr Khamis Kulemba akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani(NA SHUSHU JOEL) |
Aliongeza kuwa waandishi wa habari kote nchini wanapaswa kuandika habari za milipuko ya magonjwa kutokana na kuwa wao wana nafasi kubwa ya kueneza ujumbe kwa haraka kwenye jamii kuliko kitu kingine.
"Niwapongeze waandishi wa Mkoa wa Simiyu kwa kuamua kuniita kuja kuwapa elimu juu ya madhara ya magonjwa ya mlipuko katika jamii"Alisema Dr Kulemba.
Aidha Dr Kulemba alisema kuwa magonjwa haya ya mlipuko uleta changamoto kubwa katika jamii ikiwemo kushuka kwa uchumi wa Taifa na sababu nyingine nyingi huku akiitolea mitano kwa baadhi ya magonjwa ya mlipuko yaliyotikisa Dunia ikiwemo Corona.ugonjwa wa Tauni unaosababishwa na panya hivyo tahadhara na elimu vinatakiwa kwenda sambamba kwa jamii ili kuepukana na magonjwa hayo ya milipuko.
![]() |
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza elimu ya magonjwa ya milipuko (SHUSHU JOEL) |
Naye Bahati Sonda ambaye ni Mwandishi wa habari wa gazeti la majira kutokea Mkoa wa Simiyu amempongeza Dr Khamis na kusema kuwa elimu hiyo itawasaidia wana habari katika kutoa elimu kwa jamii.
Aidha alisema kuwa kazi iliyobaki kwa waandishi ni wakati wa kutumia kalamu zao kuhakikisha wanaisaidia jamii kupata elimu ya kutosha juu ya magonjwa ya mlipiko.
![]() |
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia elimu juu ya magonjwa ya milipuko(NA SHUSHU JOE) |
Kwa upande Anitha Bamugileki ambaye ni mwandishi wa habari wa vyombo vya uhuru media ametoa pongezi kwa mkufunzi huyo kwa jinsi alivyoshusha nondo kwa waandishi wa mkoa wa simiyu na hivyo ametufanya waandishi kuwa na uelewa mkubwa juu ya magonjwa ya milipuko.
MWISHO
0 Comments