NIDA YAWATOA HOFU WATANZANIA.

 Na shushu joel,Simiyu.

 MAMLAKA ya vitambulisho vya Taifa(NIDA) imewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania kwa ujumla juu ya upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa.

Masimamizi wa Nida Godfrey Tengeneza akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani(NA SHUSHU JOEL)Add caption

 Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la NIDA lililopo kwenye maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea Mkoani Simiyu katika viwanja vya Nyakabidi Afisa Msimamizi wa Nida Godfrey Tengeneza alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa na hofu juu ya kupata kwa vitambulisho vyao,lakini niwatoe hofu kwani serikali imejipanga na kila kitu kiko sawa na wote mtapata vitambulisho na kuvitumia pale panapohitaji

Maafisa wa NIDA wakiwahudimia wananchi wa mkoa wa Simiyu waliojitokeza kwenye banda lao kupata huduma.(SHUSHU JOEL)

 Aliongeza kuwa kwa sasa mwambaji unapoomba kitambulisho kitu cha kwanza ni kupatiwa no ya utambulisho ila baada ya muda mchache utapatiwa kitambulisho kikiwa kimekamilika.

 "Ongezeko la uhitaji linazidi kuwa kubwa ingawa tunapambana nalo kuhakikisha kila kitu kinakuwa kama ilivyopangwa"Alisema Tengeneza. Aidha amewataka watanzania kuwa waangalifu na kuvitunza vitambulisho hivyo kwani kesi za kupoteza zimekuwa nyingi kuliko wanaohitaji kuandikishwa.

Adam Sipemba Afisa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)akiwahudumia wananchi waliopoteza vitambulisho vyao.(SHUSHU JOEL)

 Pia alisema kuwa serikali imeagiza mitambo miwili kutoka nchini Ujerumani na tayari vifaa hivyo vipo ofisini Kibaha kuna wataalamu tu kutoka Ujerumani wanasubiliwa kuja kuwaelekeza wataalamu wetu ili waendelee na kazi ya uzalishaji,vifaa hivyo vinauwezo wa kuzalisha vitambulisho 144,000 kwa siku moja hivyo changamoto iliyokuwepo inakwenda kuisha kabisa.

 Kwa upande wake Adam Sipemba ambaye ni mmoja wa watumishi wa Nida anasema kuwa wananchi wanazidi kujitokeza kwenye banda letu lakini asilimia kubwa ni wale waliopoteza vitambulisho vyao. Aliongeza kuwa Nida Mkoa wa Simiyu tumejipanga kuwahudumia wakazi wa mkoa huu kwa nidhamu ya hali ya juu. 

 Aidha Sipemba amewataka wananchi kuendelea kufika ofisi za Nida kwenye wilaya zote za Mkoa huu ili kuweza kuendelea kupata huduma hata kama ifikapo kikomo cha sherehe za Nane Nane

Afisa  wa Nida Adam Sipemba akitoa huduma ya vitambulisho kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu waliojitokeza kwenye viwanja vya Nane Nane (SHUSHU JOEL)

 Naye Mabula Masunga(57) amewapongeza mamlaka ya vitambulisho Taifa(NIDA) kwa utoaji wa elimu kwa wananchi kwani wengi wetu uelewa ni mdogo hivyo uwepo wenu hapo kwenye maonyesha ya Nane Nane yanayoendelea hapa Nyakabindi.

 Pia alisema kuwa kama elimu ya vitambulisho kama itaendelea hivyo kila mwananchi atakuwa na uelewa wa kutosha. 

 MWISHO

Post a Comment

0 Comments