Na Anita Balingilaki, Bariadi
Naibu waziri wa afya ,maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Godwin Mollel kupitia wizara ya afya, amesema wizara imejipanga kuunganisha hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu na hospitali ya muhimbili kwa lengo la kuwarahisishia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi.
![]() |
Muonekano wa majengo ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu |
Hayo yamebainishwa mapema Aug 7 na naibu waziri hiyo mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya hiyo iliyopo Nyaumata mjini Bariadi.
Amesema kuwa kabla ya kuwepo kwa hospitali hiyo wagonjwa walikuwa wakilazimika kwenda nje ya mkoa ikiwemo Bugando ya jijini Mwanza kutibiwa ambapo kwa sasa wanapata huduma kwa urahisi ndani ya mkoa.
![]() |
Awali mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Festo Dugange ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka 5 ya serikali ya Dkt John Pombe Magufuli kumewepo na ongezeko la vituo vya afya kwa zaidi ya 40% kutoka 196 hadi kufikia 218 ambavyo vimepunguza tatizo la vifo vya kinamama na watoto wachanga
![]() |
Muonekano wa hospital ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kukamilika |
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali hiyo hospitali Dkt Matoke Muyenjwa ameongeza wametenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.
MWISHO
0 Comments