Na Shusghu
Joel,Simiyu.
ALIYEKUWA
katibu Tawala mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini amekili kuwa maonyesho ya Nane Nane
mwaka huu ya kanda ya ziwa mashariki yanayofanyika
mkoani Simiyu yamekuwa na vivutio vingi kwa wakulima wa mkoa huo
Jumanne Sagini akiangalia njia ya kisasa ya uhifadhi wa nyuki kutoka kwenye Banda la mkoa wa Mara.(PICHA NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza
wakati alipokuwa akizunguka zunguka kwenye mabanda mbalimbali Sagini alisema kuwa
mwaka huu imekuwa ni tofauti na miaka mingine kutokana na kuwa taasisi nyingi
zimejipanga kuonyesha uwezo wa hali ya juu kwa kwa wananchi wa mkoa huo.
“Mwaka huu
kumekuwa na fursa vyingi ambazo miaka yote miwili iliyoita haikuwai kujtokeza
kwani elimu imekuwa nyingi hivyo naamini wananchi wa Simiyu watanufaika sana na
kile kilichopo kwenye maonyesho hayo”Alisema Sagini.
Mmoja wa wauzaji wa Dagaa wasio na michanga akimuelezea Sagini jinsi ya kuanika dagaa hao pasipo kuwa na michanga.(SHUSHU JOEL) |
Aliongeza Taasisi mbalimbali zikiwemo za serikali na
zile za watu binafsi zimejitokeza kwa wingi kuonyesha kile walichonacho kwa
wananchi wa Simiyu.
Kwa upande
wake Bi,Bertha Nyambuko mara baada ya kutembelewa kwenye banda alisema kuwa
mwaka huu kuna mabadiliko makubwa ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kwani
suala la maonyesha lilikuwa geni kwa wananchi wa maeneo hayo kwani inaonekana
walizoea magulio lakini kipindi wakazi wengi wanajitokeza kwenye maonyesho na
wengi wananunua na kuulizia vitu.
Sagini akiangalia viatu kutoka kwa mjasiliamali na mtengenezaji wa viatu(SHUSHU JOEL) |
Aliongeza
kuwa viongozi wa mkoa huu nao wamekuwa wabunifu siku hadi siku hivyo ni lazima
tu watu wajae.
Naye Dotto
Luhende ambaye ni Afisa Masoko wa Taifa Gesi alisema kuwa kipindi hiki kimekuwa
na manufaa makubwa kutokana na kuwa wananchi wemekuwa na mwamko mkubwa wa kujua
thamani ya maonyesho haya.
Mh sagini akipata maelezo ya jinsi ya kufukuza ndege kwa njia ya kisasa kutoka kwa wataalamu wa kutengeneza vifaa hivyo toka chuo kikuu cha Dar es Salaam(NA SHUSHU JOEL) |
Aidha
Luhende aliongeza kuwa kama inawezekana maonyesho hayo yakaendelea mkoa huu ni
vyema zaidi kuliko kila baada ya miaka3 yanahama kwani hapa kwenye viwanja hivi
kuna uwekezaji mkubwa umefanyika hivyo serikali ilione ili.
MWISHO
0 Comments