Na Shushu Joel,Simiyu.
HALMASHAURI ya wilaya ya maswa ya Mkoani Simiyu imezidi kujizolea umaarufu kwenye sherehe za maonyesho ya nane nane yanayoendelea mkoani humo kwa kwa ufugaji wa samaki,Ng’ombe na kilimo cha Pamba.
| Baadhi ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakiangalia ufugaji wa samaki wa kisasa kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Simiyu(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na baadhi ya wakazi waliojitokeza kujionea ufugaji wa samaki Afisa Uvuvi Salum Mazige alisema kuwa samaki ni moja ya utajiri mkubwa ambao unaweza ukabadilisha maisha ya mtu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa haraka sana
| Afisa Uvuvi wa wilaya ya Maswa Salum Mazige akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye maonyesho ya Nane Nane mkoani Simiyu(NA SHUSHU JOEL) |
Aliongeza kuwa ufugaji wa samaki kwa kipindi hiki unaumuhimu sana kutokana na kuwa samaki wana nyama nyeupe ambayo imekuwa ikisisitizwa na wataalamu wa afya kuwa ndiyo nyama ambayo haisababishi magonjwa kama zilivyo nyama yingine.
| Moja ya Ng'ombe wanaopatikana katika wilaya ya Maswa na wameletwa Nane Nane ili wananchi waweze kujionea wenyewe(SHUSHU JOEL) |
Kwa upande wake Afisa mifugo wa wilaya hiyo Saba Kashilimu alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Maswa imekuwa mstali wa mbele kwenye kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa ufugaji wa mifugo wa kisasa kwa lengo la kuondokana na umasikini.
| Afisa Uvuvi akitoa elimu kwa wananchi |
Alisema ilikuwa ni chnagamoto kubwa sana kwa wilaya yetu kuweza kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kufuga ng’ombe wa kisasa na hasa chotala ambao ndio wenye faida kubwa ikiwemo za mazingira lakini kwa sasa elimu imekuwa na tija kubwa kwa wananchi wengi wa maswa kuelewa thamani ya kuwa na mifugo hao.
“Ng’ombe chotala wanafaida nyingi ikiwemo kutokupatwa na magonjwa ya milipuko hivyo tumekuwa tukiwashauri wananchi kutumia mifugo hiyo kwa makusudi ya kujikwamua kwenye umasikini”Alisema Kashilimu.
Aidha Kashilimu aliongeza kuwa maonyesho ya nane nane yamekuwa yakiwafungua macho wananchi hivyo kama inawezekana tunaiomba serikali iongeze muda wa maonyesho hayo kutokana na kuwa elimu kubwa imewafikia wananchi wa Simiyu kwa ujumla wake
| Afisa kilimo wa wilaya ya Maswa akionyesha moja ya mazo yenye tija katika wilaya ya Maswa ambalo ni zao la Pamba. |
Alisema kuwa elimu aliyoipata kwenye banda la maswa atahakikisha inafika ukerewe ili nako waweze kujifunza na kutekeleza lile aliloliona huko.
MWISHO
0 Comments