-Mgombea Ubunge aahidi Ushindi wa Kishindo kwa CCM na Raisi Dr. John Magufuli
Na shushu joel
KUELEKEA uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28 mwaka huu nchini,Chama Cha Mapinduzi , wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani imezindua rasmi kampeni zake huku Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiahidi kuendelea kufanya kazi kwa kasi kubwa zaidi katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa Halmashauri hiyo ikiwemo kusimamia miradi mipya wanayotaraji kuifanya na kumalizia viporo vilivyobakia.
Akizungumza na umati wa wananchi waliojitokeza katika ufunguzi huo Kikwete alisema kuwa kazi iliyotekelezwa katika kipindi cha kwanza cha awamu ya Tano ya Uongozi ni kubwa kutokea tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo hivyo awamu hii ya pili matarjio ni makubwa zaidi ikiwemo kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.
![]() |
Mbunge wa jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni zake katika kata ya miono huku akiwa na madiwani wa jimbo hilo.(NA SHUSHU JOEL) |
Akiongeza kwa kujiamini sana Mh.mgombea huyo aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya uongozi wake , Wamefanikiwa kuunganisha vijiji na Makao makuu ya kata zote. Kwa kuunganisha njia zote za vijiji na makao makuu ya kata katika halmashauri hiyo kumewezesha dhughuli za kimaendeleo kuwa nyepesi na taarifa kufika mapema hivyo utatuzi wa kero za wananchi kuwa mwepesi. Akizungumzia kwa upande wa Afya mh. Kikwete alieleza kuwa wamefanikiwa kutekeleza kwa asilimia 98% miradi ambayo imebadili sura ya mahitaji ya wananchi upande wa upatikanaji wa huduma za afya. Kwa sasa huduma zote za tiba zinapatikana hapa Ndani ya Chalinze kuanzia huduma za Zahanati hadi Hospitali ya wilaya ambayo inaendelea kujengwa . Huduma muhimu kama Umeme na huduma ya maji ambayo ilikuwa changamoto kubwa kwa wananchi kwa sasa sio changamoto kama ilivyokuwa miaka mitano kabla ya kuingia madarakani kwa awamu yao ya uongozi. Mheshimiwa Kikwete alisema kuwa " katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tumefanikiwa kumtua mama ndoo kichwani na kufanikiwa kuimalisha ndoa zao kwa kiasi kikubwa."
Aidha Mgombea huyo aliwataka wanachama wa chama hicho kumpigia kura za kishindo Rais Magufuli ili aweze kututumikia tena kwa kipindi cha pili kutokana na utekelezaji mkubwa wa Ilani alioufanya kwa Watanzania na hasa Wana chalinze wanyonge. Pamoja na hilo, Aliongeza kuwa wananchi sio wajinga kwani wanaona yale yanayofanyika na Mheshimiwa Magufuli kwao hivyo Chama kiendelee kuwa na imani kuwa mitano ijayo ni ya Magufuli tu na hakuna mwengine.
![]() |
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Abduluhaman Kinana akiwaombea kura madiwani wa kata ya chalinze kwa wananchi waliojitokeza kwenye ufunguzi wa kampeni.(SHUSHU JOEL) |
Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa kampeni hizo Ndg. Abdulahaman Kinana ambaye ni aliwahi kuwa katibu mkuu wa chama hicho alisema kuwa kutokana na mambo mengi ya maendeleo kufanyika kwa wananchi katika miaka mitano iliyopita ni wazo kuwa wanachalinze wana kila sababu ya kumpatia kura nyingi ili apate ridhaa nyengine kuongoza nchi na kama ikibidi Rais Magufuli angekaa tu nyumbani na kusubili kuapishwa.
"Sina wasiwasi na wananchi wa Chalinze juu ya jambo la kuwapigia kura wagombea wote wa ccm kuanzia udiwani,ubunge na urais kwani ushahidi wa mengi yaliyofanyika katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya Rais Magufuli yanaonekana hasa hapa Miono tulipo," Alisema Kinana.
![]() |
Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo.(NA SHUSHU JOEL) |
Aidha aliongeza kuwa wananchi wa jimbo la Chalinze mmepata kijana Ridhiwani Kikwete, ninamfahamu kama kijana mchapakazi, Mbunifu , mpenda maendeleo, anajyeitambua,mwenye uthubutu pale inapokuja katika kufikia matamanio ya watu wake hasa Wana chalinze, kwani ameifanya Chalinze kuwa ya tofauti kabisa na ile chalinze ya miaka ya nyuma wakati anachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo hasa kwenye Huduma za Maji, Mawasiliano, nishati ya umeme na huduma mbalimbali za jamii na hata leo wanakwenda kuwa Wilaya yenye mamlaka kamili.
Pia Kinana amewapongeza wananchi wa jimbo hilo kwa umoja,upendo na mshikamano huku akiwapongeza wote waliojitokeza katika kinyang'anyiro cha Ubunge na hata kuridhia kushiriki uzinduzi wa kampeni jimbo hilo.Mh. Kinana naye aliwashikuru wananchi wote waliojitokea kushiriki uzinduzi huo.
Naye Bi' Mwajuma Ally amewapongeza viongozi wote waliojitokeza katika uzinduzi huo wa kampeni kwa kusema kuwa bado wanaimani kubwa na chama cha ccm na Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwani chama hiki kimetutoa mbali na Mgombea Ubunge huyu amefanya mengi yanayotupa nafasi ya kumchagua tena. Aliongeza kuwa bila ccm imara na wasimamizi wazuri kama Mbunge wetu na Diwani wa kata yetu tusingekuwa hapa tulipo kwani mengi yametekelezeka kwa jamii hivyo wale wanaobeza maendeleo ya serikali hatuwataki na waende zao huko walikotoka.
![]() | |
Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete akijinadi na kuwanadi madiwani wa jimbo hilo kwa wananchi wakati wauzinduzi wa kampeni zilizofanyika katika kata ya miono |
"Miaka mingi jimbo hili limekuwa likiteseka kwa kukosa maendeleo lakini kipindi cha Mh Ridhiwani Kikwete kimetufanya kutembea kifua mbele kwani kila hitaji letu lililokuwa likitusumbua kipindi kirefu limetekelezwa kwa kiwango cha juu.
Aidha Bi,Mwajuma amewataka Wazee,Kina Mama,vijana kuepuka kudanganywa kwani mengi tunajionea juu ya utendaji wa Rais Magufuli , Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani
MWISHO
0 Comments