WANANCHI CHALINZE WAMTAKA DKT. MAGUFULI AJIANDAE KWENDA IKULU KWA KISHINDO.

Na shushu joel, Chalinze.

 WANANCHI wa kata ya Ubena, halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamemtaka Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete kufikisha salamu zao kwa Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM) Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ajiandae kwenda Ikulu kwa heshima kubwa kutoka katika Jimbo lao.

Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo kwa wananchi wa kata ya Ubena juu ya faida za kumchagua Dkt Magufuli katika uchaguzi ujao.(PICHA NA SHUSHU JOEL)
 

 Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa kata ya Ubena walipokutana na Mbunge wao kuzungumzia, kupanga na kuhamasishana kujitokeza kwa ajili ya kupiga kura ili kuwachagua viongozi wao watakao watumikia kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

 Bi'Asha Shali (45) ni mkazi wa kijiji cha Ubenazomozi alisema kuwa kina mama chalinze wamejipanga kumpatia kura za kishindo Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama hicho kuhakikisha anakwenda Ikulu bila pingamizi ya aina yeyote ile kutokana na mazuri aliyowafanyia wakinamama wa Ubena na Halmashauri ya Chalinze kwa jumla.

NA SHUSHU JOEL
 

 Aidha alisema kuwa wanawake ni jeshi kubwa katika taifa hili hivyo wote kwa pamoja tumejipanga kumrudisha Dkt John Pombe Magufuli madarakani kwa sababu kubwa ikiwa ni mchango wake katika Afya, Elimu, Maji, na Mikopo ya wakina mama. 

 Abdul Iddy ni Mwenyekiti wa kitongoji cha cha mpakani alisema kuwa Rais Dkt Magufuli amefanya mambo mengi kwa wananchi ndio maana leo wanachama wa chama cha mapinduzi(CCM) wamekuwa na uhakika wa ushindi kwa Mgombeo wa nafasi ya Urais.

 Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Ridhiwani Kikwete amewapongeza wananchi wake kwa kuonyesha umoja,upendo na mshikamano kwake katika miaka mitano iliyopita na pili kumhakikishia kumpatia kura za kishindo Mgombea wa nafasi ya Urais Dkt Magufuli. Aidha Kikwete alisema kuwa hakuna mkazi wa Chalinze asiyetambua thamani na Mchango wa Dkt. Magufuli katika Jimbo letu ndani ya kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano iliyopita

. "Miaka mingi iliyopita Jimbo letu lilikuwa na changamoto nyingi na kwa asilimia kubwa amechangia kumaliza kero hizo"Alisema Kikwete.

Pia Mbunge huyo amewakumbusha wananchi kukumbuka kuendelea kukumbuka nyuma kidogo changamoto ya maji iliyokuwa imedumu kwa kipindi kirefu,Changamoto za Afya ambazo nazo zimetatulika kwa kiasi kikubwa,Miundombinu na Umeme hivyo imani yangu Dkt Magufuli ni uhakika atangulie Ikulu kuwatumikia wananchi.

 MWISHO

Post a Comment

0 Comments