Na Shushu Joel,Chalinze.
WANANCHI wa kata ya Mbwewe,Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kutokuteteleka na uchaguzi mkuu unaokuja kwani wamejipanga kuhakikisha Mgombea wa nafasi ya Urais na Udiwani wanapata ushindi wa kishindo.
Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimia na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi(CCM) mara baada ya kumuombea kura Dkt Magufuli(PICHA NA SHUSHU JOEL)
Wakizungumza kwenye mkutano huo, wananchi hao walisema kuwa hakuna mtu asiyeona kazi za maendeleo zinazofanywa na viongozi wa CCM."Miaka mitano iliyopita imekuwa na mafanikio makubwa sana hasa kwa upande wa huduma muhimu za binadamu na tunamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge na Raisi kwa kazi Kubwa ," alisema ndugu Baruti ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kwaruhombo.
Semeni Baruti(43) aliongeza kuwa wanatambua thamani ya Rais Dkt Magufuli hivyo ni lazima tumpatie kura za kutosha ili aweze kuendelea kututumikia wanyonge kutuletea maendeleo zaidi ya miaka mitano iliyopita.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za kumuombea kura Rais Dkt Magufuli na Diwani wa kata ya Mbwewe zilizofanywa na mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete(NA SHUSHU JOEL)
Aliongeza kuwa ni kipindi kirefu kijiji chao klikuwa kimesaulika lakini tangu kuingia madarakani Mbunge wa jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete neema kubwa imekuwa ikiwadondokea wananchi wa eneo hilo ,“Tutakuwa ni wachoyo wa fadhili kama tusipompigia kura za kutosha Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli,Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete ameshapita na Diwani wetu Omary Msonde kutokana na hatua kubwa walizotufikisha wanakijiji wa Kwaruhombo”Alisema Baruti.
Kwa upande wake Mnasambwe Omary(46) alisema kuwa chama cha mapinduzi chini ya viongozi wake Raisi Dr.Magufuli na Mbunge kimefanya kazi kubwa kwa wananchi wa kata ya Mbwewe hivyo ni lazima tukipatie kura za kutosha ili kiendelee kutufanikishia maendeleo.
Aidha alimtaka mbunge Kikwete kuanza kushangilia tu kwani kazi iliyotendeka kwa miaka mitano ya Rais Dkt Magufuli ni alama tosha kwetu.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete amewapongeza na kuwashukuru wananchi hao kwa kutambua mchango mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa utekelezaji wake mkubwa wa maendeleo katika jimbo hilo.
Wananchi hao Walisema kuwa kazi kubwa iliyofanyika kwenye jimbo letu ni historia na alama ya pekee kwa Rais Magufuli na Mheshimiwa Mbunge kwani maji,Umeme,Miundombinu na Huduma za Afya zimekuwa imara zaidi kwa wananchi kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. “Mpeni kura za kishindo Rais Dkt Magufuli kwani ameonyesha dhamira kubwa kwetu sie wanyonge kwa kutuletea maendeleo ya kweli kwa jamii zetu”Alisema Kikwete.
Aidha mbali
na kumuombea kura Rais Magufuli na Diwani wa kata hiyo Bw. Omary
Msonde,Mheshimiwa Kikwete aliwataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kuwa
walinzi wa miradi na maendeleo inajengwa na serikali pamoja na wahisani
mbalimbali ili iweze kuendelea kudumu kutumika kwa kizazi kirefu zaidi.
Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akiwalimia umati wa wananchi waliojitokeza kwenye milkutano yake ya kumuombea kura Rais Magufuli.(NA SHUSHU JOEL)
Mwisho mheshimiwa Mbunge Kikwete aliwaomba wananchi kuachana na watoa maneno mengi kipindi hichi na kuangalia maendeleo yaliyofanyika katika kata yao ya Mbwewe.
MWISHO
0 Comments