AIRTEL YAFANYA KUFURU BAGAMOYO SASA NI MWENDO WA 4G

Na Shushu Joel,Bagamoyo

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel nchini imezindua huduma za mfumo wa mawasiliano kwa kutumia 4G kwenye mji wa kitalii wa Bagamoyo Mkoani Pwani kwa kusudi la kuboresha huduma za upatikanaji wa mawasiliano ya urahisi kati ya Data  na mawasiliano ya kawaida.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi, Fatuma Latu akikata utepe wa uzinduzi wa huduma ya 4G(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa duka hilo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Bagamoyo Bi,Fatuma Latu alisema kuwa kampuni ya Airtel imekuwa msaada mkubwa kwenye sekta ya mawasiliano katika halmashauri yetu kutokana kuwa kiungo kikubwa cha wananchi katika mawasiliano.

“Kwetu sisi Wana Bagamoyo kuzinduliwa kwa huduma hii ni mafanikio makubwa hivyo wananchi niwaombe tuiunge mkono kampuni hii ya Airtel kutokana na kuwa imekuwa ni msaada mkubwa kwa jamii ya Bagamoyo”Alisema Mkurugenzi Latu.

Duka la kutoa huduma za 4G lililozinduliwa wilayani Bagamoyo(NA SHUSHU JOEL)
Aidha alisema kuwa moja ya kampuni ambazo zimekuwa zikirudisha gawio kwa jamii ya wana Bagamoyo ni pamoja na Kampuni ya Airtel hivyo ameitaka kampuni hiyo kuendelea kujitoa kwa wilaya ya Bagamoyo kama inavyofanya sasa.

Kwa upande wake Meneja Biashara wa Airtel kanda ya Pwani,Brighton Majwala alisema kuwa ni vyema wananchi wa wilaya ya Bagamoyo wakachangamkia fursa hii iliyojitokeza kwao ya uwekezaji wa masafa ya huduma za 4G. kwani bora na zenye spidi ya pekee.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo akiteta jambo na baadhi ya viongozi wa AIRTEL  mara baada zoezi la ukataji utepe.
Aliongeza kuwa kampuni ya Airtel nchini iliahidi kuboresha hupatikanaji wa huduma zake nchini na hivyo tumeanza kutekeleza aahidi zetu kwa wananchi.

Naye Juma Haji ni mmoja wa wateja waliojitokeza kwenye uzinduzi huo ameipongeza kampuni ya Airtel kwa kutambua thamani ya wananchi wa Bagamoyo kwa kuwapelekea huduma iliyokuwa wakiisubili kwa muda mrefu.

Pia amewataka wananchi kuchangamkia fursa hizo kwani kwa hali hii mtandao wa Airtel utakuwa kwa kwanza kwa kasi kwenye mawasiliano na Data.

MWISHO

0717913670

 

 

 

Post a Comment

0 Comments